Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Ndugu Stafa Nashon, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya juma la ELIMU ya watu WAZIMA na ELIMU NJE ya MFUMO RASMI, siku ya tarehe 4/9/2025 alifungua maadhimisho hayo kwa kutembelea mabanda mbalimbali yaliyopo na kujionea shughuli zinazofanywa na wajasiriamali wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, kuona wanafunzi wanaopata elimu NJE ya mfumo usio rasmi jinsi walivyoweza kutumia ujuzi wao walioupata kupitia vituo vilivyopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, pia aliweza kupata elimu ya ufugaji nyuki na namna ya utunzaji wa mazingira, na pia aliweza kuona vifaa mbalimbali vinavyotumika katika kufundishia watu wenye mahitaji maalumu.
Maadhimisho ya juma la ELIMU ya watu WAZIMA yalifanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kibara, na kuhudhuriwa na wananchi mbalimbali, pamoja na wanafunzi kutoka shule za msingi na Sekondari.
Lengo kuu la kuadhimisha juma la ELIMU ni kuendelea kuimarisha elimu ndani ya mfumo RASMI na elimu NJE ya mfumo RASMI, ambao unajumuisha Madarasa ya MEMKWA, ELIMU MAALUMU SEQUIP, vituo vya ufundi, mukeja na ODL ( Open and Distance Learning) kwa walimu.
Akisoma risala kwa mgeni rasmi Mwalimu Florence Njiku alisema, jumla ya wanafunzi 371 wamerudi shuleni kupitia programu ya MEMKWA baada ya kusitisha masomo kutokana na changamoto mbalimbali, na wanafunzi 236 wenye mahitaji maalumu wameandikishwa, pia, wanafunzi 21 wakike waliokatisha masomo wamerudi kupitia program ya SEQUIP. Haya ni mafanikio makubwa yaliyotokana na uwepo wa program za elimu ya watu WAZIMA katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
" Tuna vikundi mbalimbali vya wajasiriamali na wadau wanaochangia utoaji wa elimu ya ufundi katika vituo viwili ambavyo vinapatikana Nyamuswa na Kibara." Alisema Bi. Njiku.
Ndugu Nashon, alisema tutumie teknolojia katika kufundishia watu WAZIMA na pia tujutahidi kujua kusoma na kuandika na tuongeze bidii kufungua Madarasa na vituo vya elimu.
" Kukuza kisomo katika zama za kidijitali kwa maendeleo endelevu."
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika:
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda