• Malalamiko |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Bunda District Council
Bunda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji & Ushirika
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Fedha & Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Mifugo & Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi & Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu Msingi
    • Barabara
    • Mifugo
    • Afya
    • Mazao ya kilimo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi & Mipango
      • Elimu, Afya & Maji
      • AIDS Control
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Uma
    • Video
    • Hifadhi ya Picha
    • Habari
    • Matukio

ELIMU IENDELEE KUTOLEWA KWA WANANCHI KULA VYAKULA VYENYE LISHE ILI KUPUNGUZA UTAPIAMLO

Posted on: September 5th, 2025

Kikao cha tathimini ya lishe kwa robo ya nne kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ngazi ya Halmashauri cha kupokea na kujadili taarifa mbalimbali kutoka divisheni na vitengo mtambuka vinavyoshirikiana na uhamasishaji wa lishe katika jamii, kimefanyika siku ya tarehe 4/9/2025 katika ukumbi mdogo wa Halmashauri uliopo Kibara Stoo.


Akiongoza kikao hicho, Mwenyekiti wa kikao ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu George S Mbilinyi, aliwasisitiza na kuwakumbusha divisheni na vitengo vinavyohusiana na masuala ya lishe, kuhakikisha wanahamasisha wananchi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kula vyakula vyenye lishe Bora ili kuondokana na kupunguza utapiamlo katika jamii.


" Mnapokuwa na mikutano na wananchi wenu huko hakikisheni ajenda ya lishe inasisitizwa, na sio kuishia kuhamasisha lishe shuleni tu, hata jamii zetu zinatakiwa zifahamu umuhimu wa kupata mlo kamili na ulio na lishe Bora, hapo ndio tutaweza kupunguza utapiamlo katika jamii nzima." Alisema.

Wananchi wamekuwa wakilima mazao mbalimbali lakini wengi wao unakuta hawali mlo kamili wanaishia kuuza kwa wengine huku utapiamlo ukiendelea kuongezeka katika jamii, hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha tunashirikiana kwa pamoja kuhakikisha elimu inatolewa kwa wananchi wote kuhusiana na faida za kutumia vyakula vilivyo na viritubishi kwa ajili ya kupata lishe iliyo Bora.


Ndugu Mbilinyi, alimuagiza Afisa kilimo kwa kushirikiana na Afisa Biashara kuhakikisha wanawatafutia wakulima soko la kueleweka kwa ajili ya kuuza mazao yao, hasa mazao ya bustani ambayo yameonekana wakulima wamekuwa wakilima lakini hawana soko la uhakika la kupeleka mazao yao hivyo kupelekea kukata tamaa kwa wakulima kuendelea kulima mazao hayo.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI September 07, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI September 18, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WOTE December 20, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • WATENDAJI KATA NA MIJI WAAGIZWA KUENDELEA KUWEKA MSISITIZO KATIKA UHAMASISHAJI WA UCHANGIAJI WA CHAKULA SHULENI

    September 09, 2025
  • HALMASHAURI YAADHIMISHA JUMA LA ELIMU YA WATU WAZIMA NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI

    September 05, 2025
  • ELIMU IENDELEE KUTOLEWA KWA WANANCHI KULA VYAKULA VYENYE LISHE ILI KUPUNGUZA UTAPIAMLO

    September 05, 2025
  • TMDA WATOA ELIMU KWA WATUMISHI WA AFYA JUU YA UTOAJI WA TAARIFA ZA MADHARA NA MATUKIO YA VIFAA TIBA NA VITENDANISHI.

    August 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Mvamizi wa eneo la soko.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Baraza la Madiwani
  • Dira na Dhamira
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mpango Mkakati
  • Mpango wa Uwekezaji Sekta ya Samaki
  • Muundo wa Taasisi
  • OPRAS - Form

Viunganishi Muambata

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2023 Bundadc
  • Matokeo ya darasa la saba
  • Matokeo ya darasa la saba
  • PO-RALG
  • PO-PSM
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2019

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Kibara Stoo.

    Anuani ya Posta: 126, Bunda

    Simu: 0282621055

    Hamishika:

    Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda