Kaimu Mkurugenzi Bw. Stafa Nashoni amefungua mafunzo ya TASAF kwa Wawezeshaji ngazi ya Kijiji kwenda kufanya uhakiki taarifa za wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF unayoelekeza mpango wa kuruhusu kaya masikini.
Amewataka wawezeshaji wote kufanya kazi kwa uwaminifu kutofanya upendeleo wowote,ikiwa pamoja na na kutunza vitendea kazi walivyopatiwa”Mh: Rais alishaelekeza kuwa uhakiki huu wa kipindi cha pili awamu ya tatu uwe wenye uweledi na umakini mkubwa ili kupata taarifa sahihi za walengwa katika maeneo yetu,hivyo nategemea kaya zote zitapatikana kihalali katika wilaya ya bunda”.alisisitiza
Alieleza zaidi kuwa ni muhimu kila muwezeshaji kuhakikisha anafuata muongozo na utaratibu ambao umetolewa kati kazi hiyo.
Zakaria Msomi Muwakalishi wa Mkurugenzi TASAF ameeleza malengo ya zoezi hilo kuwa ni kuondoa walengwa hewa,kujenga uelewa wa pamoja wa zoezi la uhakiki wa walengwa kwa mujibu kwa mujibu ya maelekezo ya Mhe Rais Dkt John Pombe magufuli wakati wa uzinduzi wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu TASAF.
“Uwepo wa kaya hewa katika maeneo ya utekelezaji ni aibu sana kwa viongozi wa mikoa,Wilaya na Halmashauri.Serikali haitakuwa na huruma na mtu yeyote.Kufanikiwa au kutofanikiwa kwenye maeneo yenu itakua mojawapo ya vipimo ntakavyotumia kujua kama mnastahili kuendelea na nafsi mlizonazo au la. Siwatishi lakini huo ndo ukweli.”alisema mwakilishi wa TASAF
Mafunzo hayo ya siku mbili yatafanyika katika ukumbi wa Halmshauri na wawezeshaji ni Bw. Zakaria Msomi na Bw. Elius Muyomba na ambapo jumla ya mada 9 zinatarajiwa kutumika katika mafunzo hayo.
Pamoja na hayo tathimin ya serikali ya utekelezaji wa TASAF kipindi cha kwanza awamu ya tatu inaonesha umasikini nchini umepungua kwa asilimia 10 na umasikini uliokithisiri asilimia 12.Kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini .
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda