Katika kikao kazi cha tathmini ya Maendeleo ya elimu na utoaji wa tuzo divisheni ya elimu Sekondari imetoa tuzo hasi na chanya kwa shule zilizofanya vizuri katika ufaulu wa matokeo ya kidato cha pili na cha NNE, na tuzo hasi imetolewa kwa shule iliyoshuka ufaulu kwa mwaka 2024.
Pia, divisheni ya elimu Sekondari imetoa zawadi MBALIMBALI kwa walimu na maafisa elimu kata waliosimamia vizuri shule zao na kupandisha ufaulu katika matokeo ya kidato cha pili na cha NNE KWA MWAKA 2024.
Zawadi na tuzo hizo zilitolewa siku ya tarehe 2/4/2025 katika ukumbi wa chuo cha ualimu Bunda na mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda Ndugu Salum Mtelela, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh. Aswege Enock Kaminyoge.
Ndugu Mtelela alisema lengo la kikao kazi hiki ni kutathmini maendeleo ya elimu na kuwapa motisha wale ambao wameshindwa kupata zawadi katika shule zao, ili mwakani waweze kuongeza mbinu na ufanisi ili waweze kufanya vizuri.
Zawadi hizo zilitolewa kwa shule na kwa Mwalimu mmojammoja kulingana na ufaulu wa somo lake, hivyo walimu wametakiwa kuongeza juhudi katika ufundishaji wao ili waweze kufaulisha wanafunzi wengine zaidi, nao maafisa elimu kata wametakiwa kuhakikisha wanafanya KAZI yao ipasavyo kwa kuhakikisha wanasimamia maendeleo yote ya elimu, ufuatiliaji wa watoto watoro shuleni kwa kushirikiana na Afisa Mtendaji kata na kuhamasisha suala la uchangiaji wa chakula shuleni.
Kauli mbiu: "Ufundishaji na Ujifunzaji unaozingatia malengo ni msingi wa kuongeza ubora wa ufaulu".
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda