Kamati ya usimamizi ya utoaji wa mikopo ngazi ya halmashauri, ikiongozwa na Bi. Rachel Lazaro ambaye ni Afisa Maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda siku ya tarehe 25/4/2025 imefanya ziara ya kutembelea na na kukagua vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambavyo vimeomba mkopo wa Halmashauri wa asilimia kumi kwa awamu ya pili baada ya kufungwa kwa dirisha la maombi hayo.
Bi. Lazaro alisema lengo la kufanya ziara hiyo ni uhakiki wa miradi ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na kujiridhisha na vikundi husika kulingana na thamani ya mkopo vilivyoomba kama vinauhalisia na thamani ya fedha waliyoomba kabla ya kikundi kupewa mkopo.
" Ziara hii ni ya kawaida kabisa kwa kamati zote kujiridhisha kwa kutembelea na kukagua miradi ya vikundi kabla ya kupewa mkopo, kamati za mikopo huanzia ngazi ya Kata, Halmashauri hadi Wilaya baada ya kujiridhisha kwa kamati zote hizi ndipo kikundi kilichotimiza sifa zote za kuomba mkopo hupewa kulingana na mradi husika baada ya kujiridhisha nao. Alisema Bi. Lazaro.
Kamati ya usimamizi wa mikopo ngazi ya halmashauri ilitembelea na kukagua jumla ya vikundi 55 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. katika Kata 15 za Halmashauri ya Wilaya ya Bunda zilizotuma maombi ya mkopo.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda