Wakuu wa divisheni na vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda walipewa mafunzo ya namna ya uandaaji na utengenezaji wa mpango mkakati wa Halmashauri wa miaka mitano (strategic plan).
Mafunzo hayo yalitolewa na wataalamu kutoka chuo cha mipango na maendeleo ( IRDP) Kanda ya ziwa yaliyohusisha uandaaji na utengenezaji wa mipango mkakati ambao utatoa dira na muelekeo wa Halmashauri kwa Kila divisheni na vitengo ukionesha kazi za Kila divisheni na vitengo, dira na muelekeo wa Halmashauri kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2025 hadi 2030.
Akihitimisha mafunzo hayo Dkt Daniel Mpeta ambaye ni Mkuu wa mafunzo katika chuo cha mipango na maendeleo kwa Kanda ya ziwa alisema, kazi yao kubwa ni kufanya utafiti, kufundisha na kutoa huduma sehemu mbalimbali kama kufundisha wataalamu Katika uandaaji na utengenezaji wa mpango mkakati wa Halmashauri ambao utaisaidia Halmashauri kutekeleza majukumu yake kulingana na mpango kazi na mikakati waliyojiwekea.
Dkt Mpeta, aliwashukuru washiriki wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa kuweza kushiriki katika mafunzo na kukubali kuwaalika katika utoaji wa mafunzo hayo ya namna ya uandaaji wa mpango mkakati.
Mafunzo ya uaandaji na utengenezaji wa mpango mkakati wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda yamehitimishwa siku ya tarehe 24/4/2025 na yalifanyika katika ukumbi wa Landmaster Hotel uliopo Bunda Mjini.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda