Katika kuimarisha kilimo cha zao la Pamba ambacho kilidorora kwa muda mrefu, Mkuu wa Mkoa wa Mara Ndg. Adam Kigoma Malima amezindua Shamba Darasa la zao hilo Mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanyika katika Wilaya ya Bunda ikiwakilisha eneo la majaribio kwa Mkoa huu ambapo shamba lenye vitalu 12 kila kimoja kikiwa kimetengewa hali tofauti kama vile aina ya mbegu ya pamba (yenye manyoya /isiyo na manyoya), aina ya mbolea, hali ya hewa, nk lilitumika kutoa elimu kwa Wakulima wa zao hilo ambapo kwa kiasi kikubwa Wakulima waliohudhuria tukio hilo walionekana kupata matumaini mapya katika kulima zao hilo la kibiashara kwa Kanda ya Ziwa.
Pamoja na Washiriki wengine, shamba darasa hilo ambalo liliandaliwa kitafiti zaidi ili liweze kutoa mwanga kwa wadau mbalimbali wanaojihusisha na zao hilo, Kituo cha kitafiti cha Ukiluguru cha Mkoani Mwanza, Maafisa Kilimo toka ngazi ya Mkoa na Halmashauri walishiriki kikamilifu katika kuhakikisha kuwa utaalamu wao unatumika ipasavyo na hivyo kuwanufaisha Wakulima wa zao hilo na Wananchi wa kawaida kwa ujumla wao katika kuhakikisha kuwa zao hilo muhimu kibiashara linarudi katika hadhi yake na hivyo kuwanufaisha wakulima wake hasa katika kuleta tija kwenye maisha yao.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda