Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu George S Mbilinyi amewapongeza viomgozi wote walioshinda kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, 2024 ulimalizika tzrehe 27/11/2024.
Pongezi hizo alizitoa wakati viongozi hao walipomaliza kula kiapo cha Utii na Uadilifu siku ya tarehe 29/11/2024 katika shule ya msingi Mugeta.
Ndugu Mbilinyi aliwaambia viongozi hao wanatakiwa kufuata maadili ya kazi kwa kuhakikisha wanafuata kanuni, sheria na taratibu za kazi, pia kuepukana na vitendo vya kupokea rushwa wafanye kazi kwa kufuata kanuni na taratibu na kuhakikisha wanaongoza wananchi wote kwa haki na usawa.
Msimamizi wa Uchaguzi aliwasisitiza kwenda kusimamia miradi yote ya maendeleo ambayo inaendelea kutekelezwa katika vijiji vyao na kuhakikisha wanasoma taarifa za mapato na matumizi kila robo ya mwaka katika vijiji vyao.
“Nyie ndio walinzi wa amani katika vijiji na vitongoji vyenu hakikisheni mnalinda amani ya kijiji kwa kuhakikisha mnaepuka kuwa chanzo cha migogoro katika vitongoji na vijiji vyenu”alisema Ndugu Mbilinyi
Kiapo cha utii na uadilifu kilitolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Mugeta Bi. Martha John.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda