Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, Ndugu Salum Khalfan Mtelela ameziagiza taasisi za Serikali ndani ya Wilaya ya Bunda kuhakikisha wanafata maelekezo ya kutumia nishati safi ya kupikia kabla ya tarehe elekezi iliyotolewa na Raisi wa Tanzania kwa taasisi za Serikali kuanza kuumia nishati hiyo ili kulinda mazingira na kuunga mkono kampeni ya Raisi Samia Suluhu Hassan ya matumizi Safi ya nishati ya kupikia.
Ameyasema hayo katika kilele cha mashindano ya Upandaji Miti katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda yaliyo fanyika katika Shule ya Msingi Mwibara siku ya tarehe 24/11/2024.
“Nitumie nafasi hii kuwakubusha wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 27/11/2024 ili kupiga kura na kuchagua viongozi ambao ni sahihi na wataleta maendeleo katika Halmashauri na Wilaya kwa ujumla na pia kushiriki mikutano ya kampeni za wagombea ilikubaini kiongozi yupi ni sahihi kwa upande wenu”Amesema Ndugu Mtelela
Katika mashindano hayo kulikuwa na michezo mbalimbali kama kukimbiza kuku, kuruka kamba, Mpira wa miguu pamoja na mazoezi ya viungo na washindi wa michezo hiyo walipewa zawadi mbalimbali.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bw.George S. Mbilinyi amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuunga Mkono Kampeni ya matumizi safi ya Nishati ya kupikia na utunzaji wa mazingira pamoja na kuhamasisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unao tarajia kufanyika tarehe 27/11/2024.
"Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ipo vijijini na wananchi wengi wanategemea kuni pamoja na mkaa kwaajili ya kupikia hali inayo pelekea uharibifu wa mazingira, kwahiyo tumeamua kutoa Elimu hii kwa wananchi ili waweze kuachana na matumizi ya kuni na mkaa na kuanza kutumia nishati Safi ya kupikia (GESI)"Amesema Mkurugenzi Mtendaji
Kwa upande wake Afisa kilimo na mratibu wa Mradi wa kuhimili Athari za mabadiliko ya tabia ya nchi (BCRAP) Ndugu, Johanes Bucha amesema mpaka sasa wamefanikiwa kupanda zaidi ya miti ya mbao15,218 na miti ya matunda mbalimbali ikiwemo maembe 500, mapera zaidi ya 3000 na parachichi zaidi ya 1000.
"Katika zoezi letu la upandaji wa miti tumekutana na changamoto ya mifugo holela ambayo imekuwa ikiharibu sana miche tunayopanda kwahiyo tunaomba ngazi za vijiji kuweka sheria kwa wafugaji holela na niwaombe wananchi kuendelea kumwagilia miti tunayopanda ili iweze kusitawi vizuri"Amesema Bucha.
Afisa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu, Moshi Ngombolwa amesema matumizi ya nishati isiyo Safi ya kupikia ni pamoja na kutumia mda mrefu wakati wa kupika na macho kuwa mekundu hali inayopelekea baadhi ya maeneo kuhusisha na Imani za kishirikina.
"Tunashauri wananchi kuwa makini sana katika suala zima la utunzaji wa mazingira kwahiyo tunashauri jamii ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kuanza kutumia nishati Safi ya kupikia (GESI) ili kuendana na kampeni ya Rais wa Tanzania na kutunza mazingira kwa kutokukata miti kwajili ya kuchoma mkaa na kuni za kupikia"Amesema Afisa Mazingira.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda