Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu Geoge S. Mbilinyi, ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Lishe alifungua kikao cha kamati ya lishe siku ya tarehe 25/11/2024 katika ukumbi wa Halmashauri uliopo Kibara Stoo.
Katika kikao hicho wajumbe waliweza kuwasilisha taarifa mbalimbali za robo ya kwanza kwa mwaka 2024/2025 ambapo walijadili masuala mbalimbali yanayohusiana na lishe shuleni kwa upande wa shule za sekondari na msingi zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Wajumbe walishauri walimu katika shule za msingi na sekondari\kuweza kupewa mafunzo ya lishe angalau mara nne kwa mwaka, ili waweze kuona umuhimu wa kuwapa watoto chakula kilicho na lishe bora.
Mratibu wa lishe na chakula shuleni Bi. Florence Njiku ameshauri kikao kutenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kununua mbegu za kilimo shuleni, na mawasiliano ya mara kwa mara yaweze kufanyika ili kuona kama shule zinatekeleza kilimo shuleni kwa uhakikisha wanafunzi wote wanakula chakula.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda