Wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ngazi ya vijiji na vitongoji unaotarajia kufanyika tarehe 27/11/2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda wameapishwa na kupewa mafunzo ya kanuni, maadili, taratibu na Sheria za usimamizi wa uchaguzi.
Uapisho huo umefanywa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bw.George S. Mbilinyi siku ya tarehe 23/11/2024 katika ukumbi wa Chuo cha Walimu Bunda.
Sambamba na hayo Bw.Mbilinyi amewataka wasimamizi hao kuhakikisha wanatekeleza zoezi hilo kwa usahihi na kuufanya uchaguzi kuwa wa huru na haki huku akisisitiza umuhimu wa kufuata taratibu na kanuni ili kuepusha sintofahamu zinazoweza kujitokeza.
"Mawasiliano katika shughuli yoyote ambayo tunakwenda kufanya ni muhimu sana ukiona kuna vitu huvielewi ni muhimu kuwasiliana na viongozi ili kuhakikisha tunaweka mambo sawa kwahiyo naomba kila mtu kuheshimu mawasiliano ni jambo la kawaida, lakini ni muhimu sana kwenye kazi tunayoenda kuifanya, kitu kingine nyie siyo wasemaji wa uchaguzi endapo mtu atakuja kuuliza jambo lolote kuhusu uchaguzi mwambie awasiliane na mimi"Amesema Msimamizi wa Uchaguzi.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa Mafunzo hayo, Ndugu Morris Johnson amesema ni vyema kwa wasimamizi wa vituo vya kupiga kura kujua taratibu za kupiga kura ambazo zinapatikana katika kanuni za kupiga kura kuanzia kanuni namba 31 hadi 37, na kuongeza kuwa vituo vya kupigia kura siku ya tarehe 27 mwezi 11 mwaka 2024 vitafunguliwa rasmi kuanzia muda wa saa mbili kamili asubuhi na kufungwa saa kumi kamili jioni.
“Niwakumbushe kuwa baada ya mtu yeyote kupiga kura hatarusiwa kubaki kwenye eneo la kituo cha kupigia kura isipokuwa anarusiwa kukaa umbali wa mita 100 kutoka kilipo kituo cha kupigia kura lakini pia tuzingatie usalama wa mpiga kura na usiri kwa mpiga kura”Amesema Ndugu Johnson.
Kwa uapande wao Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 wamesema mafunzo hayo yatawasaidia katika hatua zote za uchaguzi kuanzia zoezi la kupiga kura hadi kutangaza matokea ya uchaguzi na kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa ufanisi na kufuata sheria.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda