Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Ndugu George S. Mbilinyi amewapongeza watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa ushirikiano wa pamoja katika utendaji wa kazi kwa kuweza kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kuhakikisha tunavuka lengo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Pongezi hizo alizitoa wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri kilichofanyika siku ya tarehe 2/7/2024, katika ukumbi wa mikutano ulipo Kibara Stoo.
“Lengo kuu la kufanya kikao hiki ni kwa ajili ya kujengana na kupata tathimini ya mapato kwa mwaka wa fedha 2023/2024, changamoto zote za mwaka jana mlizopitia tushirikiane kwa pamoja ili tuone ni namna gani tutaweza kuzitatua changamoto hizo.” Alisema Mkurugenzi
Naye, Mhasibu wa Mapato wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Ndugu Mtaki Zakaria Nyaganwa alisoma taarifa ya tahmini ya mapato kwa mwaka wa fedha 2023/2024 na kusema tuna haki ya kujipongeza kwa kazi nzuri tuliyoifanya ya ukusanyaji wa mapato hadi kufikia Tshs 1,905,622,929.16 sawa na asilimia 97.4 ambazo hazijawahi kufikiwa tangu Halmashauri hii ilipogawanywa. Hizi ni juhudi za pamoja zilizofanywa na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, watumishi na wakusanya mapato wote, hivyo kujipongeza ni haki yetu sote.
“Kupitia kikao kazi hiki, tunatarajia kutoa dira ya ukusanyaji mapato kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo Halmashauri tumejipanga kukusanya kiasi cha Tshs 2,517,285,572 ikiwa Tshs 1,955,848,000 ni mapato yasiyolindwa na Tshs 561,437,572 ni mapato lindwa. Hizi ni fedha nyingi na kwa mara ya kwanza Halmashauri tumejipanga kukusanya ndani ya mwaka wa fedha 2024/2025.” Alisema Ndugu Nyaganwa.
Mkurugenzi Mtendaji aliwapongeza watumishi wote kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kuweza kufikisha asilimia 97.4 ya ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2023/2024. Tujitahidi kuongeza juhudi na ushirikiano katika kuhakikisha tunasimamia ukusanyaji mapato na kufikia lengo tuliloliweka.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda