• Malalamiko |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Bunda District Council
Bunda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji & Ushirika
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Fedha & Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Mifugo & Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi & Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu Msingi
    • Barabara
    • Mifugo
    • Afya
    • Mazao ya kilimo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi & Mipango
      • Elimu, Afya & Maji
      • AIDS Control
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Uma
    • Video
    • Hifadhi ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DIVISHENI YA ELIMU YA AWALI NA MSINGI YAFANYA TATHIMINI MTIHANI WA DARASA LA SABA NA MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA NNE.

Posted on: February 28th, 2025

Divisheni ya elimu ya Awali na Msingi ya  Halmashauri ya Wilaya ya Bunda wamefanya kikao kazi cha tathimini ya Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi darasa la saba (PSLE) na mitihani ya upimaji wa darasa la nne kwa mwaka 2024.

Kikao hicho kimefanyika siku ya tarehe 28/02/2025 katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Bunda, lengo kuu likiwa ni kujitathimini kiutendaji na kupanga namna sahihi ya mapinduzi ya elimu baada ya Halmashauri kushuka kwa asilimia 1.7 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2023.

Akiwasilisha taarifa za matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2024 Afisa taaluma wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bi. Restituta Malima amesema jumla ya wanafunzi 7851 walisajiliwa kufanya mtihani wa darasa la saba waliofanya mtihani ni wanafunzi 7157 sawa na asilimia 1.7 na kati yao waliofaulu ni  5,390 na kupelekea Halmashauri kuwa na ufaulu wa asilimia 76.

Akizungumza, Afisa Elimu ya Awali na Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bw.Deusdedith Bimbalirwa amewataka walimu wakuu wa shule za msingi kutumia muda mwingi katika vituo vyao vya kazi ili kufuatilia ufundishaji wa walimu na ufaulu wa wanafunzi.

"Walimu wakuu mmekuwa mkitumia muda mwingi kufuatilia mambo ya kiofisi kuliko kuhudhuria katika vituo vyenu vya kazi, hivyo basi niwaombe majukumu hayo ya ufuatiliaji wa taarifa za kiofisi wakabidhiwe wahasibu na walimu wengine na badalayake nyie mshinde katika vituo vyenu vya kazi ili kufuatilia zaidi ufaulu wa wanafunzi."Amesema Afisa Elimu

Kwa upande wake Mdhibiti ubora wa shule Ndugu Anthony Kazungu amesema miongoni mwa sababu zinazopelekea kushuka kwa ufaulu ni pamoja na walimu kutumia mbinu za kufundishia zilizopitwa na wakati, utoro wa walimu na wanafunzi pamoja na walimu wakuu kuwa na migogoro na walimu wengine.

Aidha, amewataka walimu kujitambua kwa kuzingatia kiwango cha ufundishaji wanapokuwa darasani na kuongeza maarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo vitabu.

Naye, mwakilishi wa Katibu tume ya walimu Ndugu,Charles Bisasaba amewataka walimu kuwa mfano bora na kujiepusha na tabia za ajabu ikiwemo mavazi yasiyofaa, utoro kazini, uchelewaji na migogoro midogomidogo huku akiwasisitiza kuwa miongoni mwa tabia ambazo hazitafumbiwa macho ni pamoja na mahusiano ya kimapenzi kati ya walimu na wanafunzi.

Hata hivyo walio hudhuria katika kikao hicho ni Afisa elimu Awali na Msingi,Afisa taaluma Awali na Msingi,maafisa elimu kata pamoja na walimu wakuu wa shule za msingi.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI June 04, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI September 18, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WOTE December 20, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ELIMU YA UTUNZAJI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA YATOLEWA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MWIBARA

    June 04, 2025
  • ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

    June 03, 2025
  • ELIMU IENDELEE KUTOLEWA KWA VIJANA RIKA BALEHE.

    May 31, 2025
  • WAUGUZI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

    May 30, 2025
  • Angalia zote

Video

Mvamizi wa eneo la soko.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Baraza la Madiwani
  • Dira na Dhamira
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mpango Mkakati
  • Mpango wa Uwekezaji Sekta ya Samaki
  • Muundo wa Taasisi
  • OPRAS - Form

Viunganishi Muambata

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2023 Bundadc
  • Matokeo ya darasa la saba
  • Matokeo ya darasa la saba
  • PO-RALG
  • PO-PSM
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2019

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Kibara Stoo.

    Anuani ya Posta: 126, Bunda

    Simu: 0282621055

    Hamishika:

    Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda