Friday 26th, April 2024
@Wilaya ya Bunda
Wakati Mwenge wa Uhuru ukiendelea na mzunguko wake katika maeneo mbalimbali nchini, Mwenge huo unatarajiwa kufika Wilayani Bunda tarehe 23/08/2017 ambapo Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Lydia Bupilipili anatarajiwa kuupokea na kuukabidhi kwa Mkurugenzi Mtendaji (W) Ndg. Amos Kusaja ambaye naye ataukabidhi Mwenge huo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Bi Janeth Mayanja mnamo tarehe 24/08/2017. Ukiwa katika halmashauri ya Wilaya ya Bunda, pamoja na mambo mengine Mwenge huo unatarajiwa kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo, kukagua vikundi mbalimbali vya kiuchumi vya Vijana na Wanawake, wakati huo huo ukiwa unatoa ujumbe mahsusi wa mbio hizo kwa Mwaka huu wa 2017 unaosema "Shiriki kukuza Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi yetu" kabla ya kukabidhiwa kwa halmashauri ya Mji wa Bunda.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754821313
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda