Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh. Dkt Vicent Anney ameongoza kamati ya usalama ya wilaya ya Bunda siku ya tarehe 30/7/2024 kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya wilaya ya Bunda, hasa upande wa jimbo la Bunda.
Mh. Dkt Anney alitembelea na kukagua maboresho ya tanki la maji lililopo katika kituo cha Afya Hunyari, ambapo siku chache zilizopita alitoa maagizo ya kwamba lirekebishwe sehemu zote zenye mapungufu ili watumishi na wagonjwa wanaohudumiwa katika kituo hicho waweze kupata huduma ya maji.
Kamati ya usalama pia ilitembelea na kukagua ujenzi wa tanki la maji katika shule ya sekondari Mariwanda, ambapo walimuagiza Muhamdisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu Timothy Mwanjala kuhakikisha anawasimamia mafundi wanaojenga tank hilo, ili liweze kukamilika kwa viwango sahihi na kwa wakati.
Pia, kamati ilitembelea na kukagua ujenzi wa njia ya kutembelea wagonjwa katika kituo cha Afya Hunyari, ambapo ujenzi upo hatua ya ukamilishaji ya upakaji rangi nguzo na kupaua.
Katika ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya na kamati ya usalama, waliongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Ndugu George S. Mbilinyi, pamoja na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda