Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh.Dkt Vicent Anney amewataka watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kushiriki kwenye zoezi la upigaji kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika tarehe 27/11/3024 na kuhudhuria mikutano ya kampeni za wagombea katika mitaa na vijiji wanavyo kaa.
Ameyasema hayo siku ya tarehe 13/11/2024 katika mkutano wa Baraza la madiwani uliofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda huku lengo kuu likiwa ni kujadili taarifa za robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025.
Amesema ni muhimu watumishi wa umma kushiriki vyema katika zoezi la uchaguzi ili wawe mfano bora kwa wananchi wengine huku akiwahimiza kuwa wahamasishaji wa zoezi hilo, sambamba na hayo ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa ukusanyaji bora wa mapato ya ndani toka kuanzishwa kwa Halmashauri hiyo na kuwahimiza kuendelea na kasi hiyo katika ukusanyaji wa mapato.
"Watumishi wengi wa umma wamekuwa na tabia ya utoro kazini hali ambayo inarudisha nyuma utendaji kazi, hivyo niwaombe kila mtu awajibike Kadri awezavyo na tuache tabia ya kupoteza mda pasipo kufanya kazi kila mtu ana takiwa kutambua wajibu wake ili tushirikiane kwa pamoja tuweze kuleta maendeleo katika Halmashauri na Wilaya ya Bunda kwa pamoja"Amesema Dkt Anney
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bw.George Mbilinyi amesema kampeni za kujinadi kwa wagombea wa ngazi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa zitaanza tarehe 20,hadi tarehe 26 ya mwezi huu 2024 na amewaomba Madiwani kutumia nafasi zao kuwahamashisha wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya zoezi la upigaji kura.
"Kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambao utafanyika tarehe 27/11/2024 zitaanza rasmi tarehe 20 na kukamilika tarehe 26 ya mwezi huu na kama kunachangamoto yoyote kuhusu uchaguzi fika Ofisi ya uchaguzi ipo wazi na tutatatua hizo changamoto"Amesema Mkurugenzi Mtendaji.
Aidha mwakilishi wa Katibu Tawala wa mkoa wa Mara Ndugu Samson Wilium amesema kuelekea mchakato wa maandalizi ya bajeti ya fedha kwa mwaka wa fedha unaokuja ameitaka halimashauri ya Wilaya ya Bunda kutoa kipaumbele kwa miradi ya ndani ya Halmashauri kwa manufaa ya Wananchi ambayo italeta tija kwa ukamilifu wake pia amehimiza kuongeza juhudi katika kusimamia miradi yote ambayo imeanza kutekelezwa ili ikamilike kwa wakati na ubora wa juu.
Hata hivyo Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda wameziomba baadhi ya tasisi za serikali ikiwemo Tanesco, Ruwasa na Tarura kuandaa mikakati sahihi ya kutatua changamoto ya maji, umeme na barabara ambazo zimekuwa zikiendelea kujitokeza ndani ya Halmashauri hiyo.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda