Kikundi cha wakulima wa mbogamboga katika kijiji cha Mumagunga ambao ni wanufaika wa mradi wa kuhimili athari za mabadiliko ya Tabianchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda siku ya tarehe 24/9/2024 walifanya ziara ya mafunzo kwa kutembelea Kata ya Kasuguti.
Jumla ya wanachama 15 wakiongoza na mratibu wa mradi Ndugu Johannes Bucha walitembelea kikundi cha Amani kilichopo Kata ya Kasuguti kwa lengo la kujifunza kilimo cha mbogamboga na umwagiliaji kwa njia ya matone.
Afisa Kilimo wa Kata ya Kasuguti Ndugu Mbinza Chokola Kuzenza aliwafundisha namna ya kuandaa shamba kwa ajili ya kilimo cha mbogamboga, namna ya kusia mbegu kwenye vitalu, namna ya kutambua wadudu waharibifu katika zao la nyanya na jinsi ya kuzuia wadudu hao.
Wanufaika waliweza kutembelea shamba la nyanya na matikiti maji ambayo yanamwagiliwa kwa njia yam atone, pia, walitembelea kitalu cha mbegu za nyanya na kuona jinsi zinavyokuzwa katika vitalu kabla ya kupelekwa shambani kupandwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda inatekeleza na kusimamia mradi wa kuhimili athari za mabadiliko ya Tabianchi, chini ya ufadhili wa mfuko wa Kimataifa wa kuhimili athari za mabadiliko ya Tabianchi (Adaptation Fund) ambao unasimamiwa na baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC).
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda