Halmashauri ya Wilaya ya Bunda siku ya tarehe 14/6/2025 iliandaa bonanza la michezo lilichezwa katika viwanja vya shule ya msingi Mwibara, ambalo lilishirikisha Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Bunda Mji na Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Halmashauri tatu zilishiriki katika michezo ya mpira wa miguu, mpira wa Pete na wavu, Halmashauri hizo ni Rorya, Bunda mji na Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambao ndio walikuwa wenyeji wa bonanza Hilo la michezo.
Afisa michezo wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu Elisha Swalle alisema, bonanza hili la michezo lilichezwa ni maandalizi ya kushiriki katika mashindano ya SHIMISEMITA, yanayotarajiwa kuchezwa Jijini Tanga mwezi wa Nane, 2025.
Ndugu Swalle aliwaomba watumishi kuendelea kufanya mazoezi ya kutosha ili siku ya mashindano ikifika waweze kushiriki vyema kwa michezo yote mpira wa miguu, Pete, na wavu.
Katika bonanza timu ya watumishi ya Rorya iliibuka mshindi wa kwanza, nafasi ya pili ilishikiliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, huku Halmashauri ya Bunda mji ikishika nafasi ya tatu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu George S Mbilinyi aliwashukuru washiriki wote walioshiriki kucheza michezo hiyo na alisisitiza watumishi waendelee kufanya mazoezi ya kutosha na sio kusubiria siku ya mashindano ndio wafike uwanjani.
Naye, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Ndugu, Potter Mtaka, alimshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa mapokezi mazuri waliyoyapata na ushirikiano wakati wote wa bonanza.
Ndugu Mtaka alisema wamefurahishwa na bonanza Hilo na waliahidi kurudi Tena Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa ajili ya Bonanza lingine, alisema, wao wapo tayari kushiriki muda na mahali popote kwani michezo ni Afya, ajira na pia inajenga mahusiano na ushirikiano mzuri baina ya watumishi na watumishi.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika:
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda