Shirika la Msaada la Marekani (USAID), likishirikiana na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI siku ya tarehe 21/11/2023 waliutambulisha mradi wa KIZAZI HODARI, katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Naibu Mkurugenzi wa mradi, Bi. Vaileth Mollel alisema, lengo la mradi huu ni kuwahudumia watoto wote walioathirika na Virus vya UKIMWI, pamoja na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.
Bi. Mollel alisema, mradi huu ni wa miaka mitano na unatekelezwa katika mikoa Tisa iliyopo Kanda ya Kaskazini Mashariki, katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda lengo ni kuwafikia watoto 1761 kwa mwaka.
Malengo makuu ya mradi huu ni kuhakikisha watoto wote waliopo katika kaya hatarishi ambao wameathirika na maambukizi ya virus vya UKIMWI kuhakikisha Afya zao zina imarika, kwa kuhakikisha wanakula vyakula vilivyo na lishe bora na kwa wakati sahihi.
“Tunahamasisha jamii kwenda kupima na kujua wangapi wamekutwa na virus vya UKIMWI na kuwashauri kuanza kutumia dawa za kufubaza virus vya UKIMWI. Pia, tuna wahudumia watoto wachanga ambao wamezaliwa na mama mwenye maambukizi ya virus vya UKIMWI kwa kuhakikisha mama zao wanawanyonyesha bila ya kupata maambukizi ya virus vya UKIMWI.
Hatutaki kuona watoto wanapitia ukatili wowote wa kijinsia kwa kuwanyanyapaa waathirika, tunafanya kazi mashuleni, nyumbani, kwa kupita nyumba hadi nyumba kufahamu watoto wangapi wanaishi katika kaya hizo hatarishi, pamoja na mitandao ya kidini”. Alisema Bi. Mollel.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Bi. Changwa M. Mkwazu aliwashukuru wadau wote pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuja kuutambulisha mradi, na alisema, tumeupokea mradi huu na tunawaahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha kwa kuhakikisha tunausimamia na kutekeleza yale ambayo mtatuambia, mapungufu yoyote yatakayojitokeza tunaahidi tutayarekebisha.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda