Timu ya Veterans wa Kibara waliibuka kidedea kwa kuwanyuka bao 3-2, timu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, katika mechi ya kirafiki iliyochezwa siku ya tarehe 20/7/2024 katika uwanja wa shule ya msingi Mwibara.
Lengo la kuwa na mechi hii ni kwa ajili ya kujenga mahusiano na ushirikiano baina ya wananchi na watumishi wa Halmashauri katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu George S. Mbilinyi, amewapongeza wachezaji wa timu zote mbili kwa ushirikiano mzuri waliounyesha katika mechi, na amewasisitiza wananchi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kuhakikisha wanajitokeza na wanashiriki kwa wingi katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, ambapo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mwenge wa uhuru tutaupokea tarehe 2/8/2024 na kuukimbiza katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ndugu Mbilinyi aliwasisitiza wananchi kujitokeza na kushiriki kwa wingi katika zoezi la uboreshaji na uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura, pale zoezi hilo litakapoanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, ili kuweza kuwachagua viongozi walio bora na sahihi katika kuwaletea maendeleo.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda