• Malalamiko |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Bunda District Council
Bunda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji & Ushirika
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Fedha & Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Mifugo & Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi & Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu Msingi
    • Barabara
    • Mifugo
    • Afya
    • Mazao ya kilimo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi & Mipango
      • Elimu, Afya & Maji
      • AIDS Control
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Uma
    • Video
    • Hifadhi ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA YAZINDUA RASMI BODI YA AFYA.

Posted on: January 9th, 2025

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda Ndugu Salum Khalfan Mtelela kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh.Dkt Vincent  Anney, siku ya tarehe 8/1/2025 amezindua rasmi bodi ya Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, ambayo itaongoza kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.

Katibu wa bodi ya Afya, ambaye ni Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Dkt. Hamidu Adinani alisema lengo la kuundwa kwa bodi ya Afya ni kwa ajili ya kusimamia huduma zote za Afya  kwa kuhakikisha watoa huduma ya Afya kuanzia ngazi za vituo, na hospitali wanatekeleza majumu yao kwa kufuata kanuni, taratibu na Sheria za utendaji kazi, ili kupunguza na kuondoa changamoto mbalimbali ambazo jamii inakabiliana nazo kwa upande wa huduma ya Afya.

Dkt Adinani alisema,  jukumu kubwa la bodi ya Afya ni kuhakikisha wanasimamia na kuhakikisha huduma za Afya zinaboreshwa kwa kuwahamasisha na kuelimisha jamii kujiunga na huduma za bima ya Afya ili waweze kupunguza gharama za matibabu pale wanapoenda katika vituo vya Afya na hospitali kwa ajili ya kupata huduma.

" Kusimamia bodi za Afya ndogo,  ambazo zipo katika  vituo vya Afya kwa kuhakikisha zinatekeleza majukumu yao ipasavyo, kusimamia mapato ya vituo vya Afya kwa kuhakikisha yanakusanywa kwa usahihi, kuwashauri mama wajawazito kujiunga na huduma ya M- mama kwa ajili ya kupata huduma ya haraka kwa kupiga  namba ya simu Bure ya 115." Alisema Dkt Adinani.

Aidha, Ndugu Mtelela ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa bodi alisema, dhima ya bodi hii ni kuhakikisha inasimamia huduma ya Afya katika Halmashauri na kuhakikisha zinaboreshwa ili wananchi waweze kuhudumiwa vizuri.

" Tuhakikishe tunawasimamia vyema wahudumu wetu wa Afya, ili kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa umakini kwa kufuata Sheria, kanuni na taratibu za taaluma zao. Tukahamasishe wananchi ili waweze kujiunga na huduma ya bima ya Afya ya iCHF, tukatimize majukumu yetu kama muongozo wa bodi ya Afya unavoelekeza, tufanye kazi kwa umoja na ushirikiano ili kuhakikisha bodi hii inatimiza malengo yake kwa kuhakikisha huduma za Afya katika Halmashauri zinaboreshwa." Alisema Ndugu Mtelela.

Katika uzinduzi wa bodi wajumbe walifanya uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti ambaye ataongoza kwa kipindi cha miaka mitatu, na uchaguzi ulifanyika kwa wajumbe kupiga kura na kumchagua Bi. Immaculata Maina kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.



Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI KWA NAFASI ZA UDEREVA May 07, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI September 18, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WOTE December 20, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYATEMBELEWA NA KUKAGULIWA NA KAMATI YA MIKOPO NGAZI YA HALMASHAURI

    April 26, 2025
  • WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAHITIMISHA MAFUNZO YA SIKU 5 YA UANDAAJI NA UTENGENEZAJI WA MPANGO MKAKATI

    April 25, 2025
  • PROJECT ZAWADI YAIPIGA TAFU MASHINDANO YA UMITASHUMTA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA

    April 07, 2025
  • WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAPEWA TUZO NA ZAWADI .

    April 03, 2025
  • Angalia zote

Video

Mvamizi wa eneo la soko.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Baraza la Madiwani
  • Dira na Dhamira
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mpango Mkakati
  • Mpango wa Uwekezaji Sekta ya Samaki
  • Muundo wa Taasisi
  • OPRAS - Form

Viunganishi Muambata

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2023 Bundadc
  • Matokeo ya darasa la saba
  • Matokeo ya darasa la saba
  • PO-RALG
  • PO-PSM
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2019

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Kibara Stoo.

    Anuani ya Posta: 126, Bunda

    Simu: 0282621055

    Hamishika: 0742163056

    Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda