Wajumbe wa kikao cha kamati ya usimamizi wa mradi wa kuhimili athari za mabadilo ya Tabianchi (BCRAP) siku ya tarehe 14/5/2025 wamefanya kikao cha uwasilishwaji na kujadili tàarifa mbalimbali za utekelezaji wa mradi kwa kipindi cha kuanzia Julai 2024 hadi April 2025.
Katika kikao hicho wajumbe wanaosimamia mradi waliweza kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa mradi ambazo waliwasilisha taarifa ya ufugaji wa samaki katika Kijiji cha Mchigondo na Isanju, taarifa ya ufugaji wa kuku katika vikundi nane, taarifa ya mashamba darasa ya kilimo, pamoja na taarifa ya Maji.
Wajumbe walizijadili taarifa hizo pamoja na changamoto zilizojitokeza katika mradi huo, ambapo ilionekana baadhi ya wanufaika wa mradi huo wameshindwa kusimamia na kuendeleza vikundi kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha pamoja ufuatiliaji wa Mara kwa mara katika usimamizi wa miradi hiyo.
Wajumbe waliazimia wasimamizi wote wanaosimamia mradi kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu mara kwa mara kwa vikundi vyote kuanzia ufugaji samaki, kilimo na mifugo ili waweze kuwa na uelewa wa kutosha katika kusimamia miradi hiyo na kuwa na tija katika jamii inayowazunguka.
Pia, wajumbe wa kikao waliazimia kuwepo na ufuatiliaji wa karibu katika vikundi vinavyofaidika na mradi huo ili waweze kuuthamini mradi na kutekeleza kwa tija waweze kupata mafanikio yao kiuchumi na kijamii kwa ujumla katika kuhakikisha miradi yote inakuwa na tija kwao na endelevu katika jamii nzima.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu Stafa Nashon aliwashukuru wajumbe kwa kuhudhuria kikao na kujadili taarifa zote kwa umakini mkubwa, na pia aliomba yale yote yaliyojadiliwa na kuazimiwa katika kikao yaende yakafanyiwe kazi.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika:
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda