Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kupitia kitengo cha Ustawi wa jamii imetoa elimu kwa watu wenye ulemavu waishio katika kata ya Chitengule, Igundu na Iramba, kuhusiana na namna wanavoweza kupata haki zao za msingi katika jamii, na kutoa taarifa pale wanapoona hawa tendewi haki kwenye jamii inayo wazunguka.
ELIMU hiyo ilitolewa siku ya tarehe 5/11/2024 na Afisa Ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bi. Maria John alisema watu wenye ulemavu wanayo haki ya kuomba na kupata mkopo unaotolewa na Halmashauri, wanayo haki ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa hivyo hawatakiwi kubaki nyuma kwa kujiona kama wao wapo tofauti na watu wengine.
Bi. Maria aliwasisitiza watu wenye ulemavu kutoka Halmashauri kuhakikisha wanashiriki katika shughuli zote za kijamii katika kuhakikisha wanajiletea maendeleo yao ya kiuchumi, na kijamii pia kwa kuhakikisha wanashiriki katika kuomba mikopo inayotolewa na Halmashauri na kushiriki kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa, hivyo aliwaomba kujitokeza kwenda kupiga kura ili waweze kuchagua kiongozi aliye Bora na sahihi ambaye watashirikiana katika kuleta maendeleo na kufikisha mahitaji yao sehemu husika, watu wenye ulemavu wanayo haki ya kusikilizwa na kushiriki katika masuala yote yanayohusu jamii.
Naye, Afisa Maendeleo ya Jamii Ndugu Justin Mtopwa aliwafundisha namna ya kuunda vikundi kwa ajili ya kupata mkopo unaotolewa na Halmashauri, hivyo aliwasisitiza kuhakikisha wanaunda vikundi kwa ajili ya kuchukua mkopo kwa Awamu ya pili dirisha litakapofunguliwa upya.
Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye ulemavu Tanzania katika Wilaya ya Bunda Ndugu Sabasaba Mseveni Haji aliwaomba watu wenye ulemavu kuhakikisha wanashiriki katika kugombea nafasi mbalimbali za uchaguzi kuanzia kwenye chama Chao cha CHAWATA, na wanashiriki kwenda kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ajili ya kuchagua viongozi walio sahihi ambao watashirikiana nao katika kuwasikiliza na kuwaletea maendeleo katika Kijiji na kitongoji.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda