Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu George S. Mbilinyi siku ya tarehe 17/1/2025, ameongoza timu nzima ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Jimbo la Bunda.
Walitembelea na kukagua ujenzi wa nyumba za watumishi zinazojengwa katika shule ya Sekondari Mariwanda na shule ya msingi Sabasita.
Ambapo, nyumba zote hizo zipo katika hatua za ufungaji wa lenta na kupauliwa.
Timu ilitembelea na kukagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Amali iliyopo katika Kijiji cha Manchimweru kilichopo katika Kata ya Mihingo ambapo ujenzi wake upo katika hatua mbalimbali za msingi, pia walitembelea ujenzi wa shule ya msingi Nyansirori ambapo ujenzi wa shule mpya unaendelea na hadi sasa wapo katika hatua za ujenzi wa msingi,
Ukamilishaji wa bweni la shule ya Sekondari Mihingo na Nyamang'uta ambapo mabweni hayo yapo hatua za mwisho za ukamilishaji ili kuweza kupokea wanafunzi, pamoja na ukaguzi wa vitanda.
Pia, timu iliembelea shule ya Sekondari Chamriho na kukagua ukamilishaji wa bweni Moja la wasichana, pamoja na ujenzi wa mabweni mapya manne yanayoendelea kujengwa katika shule hiyo, huku ujenzi ukiwa katika hatua tofauti, za ujenzi.
Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji aliwaagiza Afisa Elimu Sekondari na msingi kuhakikisha wanawasimamia mafundi katika miradi hiyo ili kuhakikisha wanaongeza Kasi ya ujenzi na kukamilisha kwa wakati, huku akiwaagiza kuhakikisha wanamshirikisha Mhandisi wa Halmashauri ili aweze kuwasaidia katika usimamizi wa majengo ili yaweze kujengwa kwa viwango imara na kwa kufuata ramani sahihi kama inavoelekeza katika majengo hayo.
Hatahivyo, walitembelea shule ya msingi Salama A na kukagua ukamilishaji wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita ya vyoo.
Mbali na kutembelea miundombinu ya elimu, pia walitembelea na kukagua hospitali ya Wilaya iliyopo Kijiji cha Bukama, ambapo alimuagiza Mganga Mfawidhi wa Hospitali kuhakikisha wanasimamia vyema hatua za ujenzi kwa hospitali, na alimuagiza Mtendaji wa Kijiji kuhakikisha anaitisha mkutano wa Wananchi ili waweze kuchagua wajumbe wa Kamati ambao watasimamia hatua zote za ujenzi na kuhakikisha wajumbe wanapewa mafunzo ya usimamizi wa miradi na namna ya kutumia mfumo wa manunuzi NeST.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda