Katika kikao cha maafisa ugani kilichofanyika siku ya tarehe 20/11/2025 katika ukumbi wa Halmashauri, uliopo Kibara Stoo, wametakiwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa kufuata kanuni, Sheria na taratibu za kazi zao.


Lengo kuu la kuitisha kikao hicho, ni kwa ajili ya kutambuana kwa watumishi wapya na waliopo, kuelezwa kanuni za kiutumishi, kupokea maagizo ya serikali, kujadili masuala ya kijamii, namna ya ukusanyaji wa mapato, kupokea taarifa kwa Kila sekta, yaani kilimo, mifugo na uvuvi.


Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, ambaye ni mratibu wa zao la pamba, Ndugu.Mashaka Mashimba alisema, katika msimu wa mazao uliopita wa mwaka 2024/2025 Halmashauri ilipata jumla ya kilo 3,104,733 kutoka katika AMCOS 48 zilizopo katika Halmashauri, hivyo kupitia sekta ya kilimo iliweza kuchangia mapato ya ndani ya Halmashauri kiasi cha Tshs Milioni 113,633.227.8.


Hivyo, basi nyie maafisa ugani kwa upande wa kilimo mnalojukumu kubwa la kuwasimamia wakulima wote ili tuweze kuvuka lengo kwa mwaka 2025/2026, kuhakikisha mnatoa elimu ya kilimo cha kisasa na chenye tija, ili wakulima waweze kunufaika na mazao wanayolima.

Naye, Mwekahazina wa Halmashauri, CPA Denary Gimirey, aliwaomba na kuwasisitiza maafisa ugani hao, kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja katika suala zima la ukusanyaji wa mapato, kwa kuhakikisha wanaisimamia vyema minada yote iliyopo ndani ya Halmashauri inakusanya ushuru unaotakiwa, kwa upande wa uvuvi napo pamoja na sekta ya kilimo.

" Suala la ukusanyaji wa mapato ya halmashauri ni letu sote, hivyo wote kwa pamoja tunapaswa kushirikiana ili tuweze kutimiza lengo la ukusanyaji wa mapato." Alisema CPA Gimirey.

Kwa upande wa masuala ya kiutumishi, Afisa utumishi wa Halmashauri Ndugu. Modestus Chama aliwaeleza na kuwakumbusha maafisa ugani wote haki na wajibu wa Kila mtumishi pale anapokuwa kazini, ikiwemo kuhakikisha anafika kazini kwa wakati na kutimiza majukumu yake kama alivyoelekezwa na mwajiri wake, pia walielekezwa haki zao za kuomba likizo na masuala mengine ya kiutumishi.

Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika:
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda