Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bw. George S. Mbilinyi siku ya tarehe 19/02/2025 ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya elimu inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri kwa lengo la kuona maendeleo na kuhakikisha miradi hiyo inajengwa kwa ubora na kukamilika kwa wakati.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji aliongozana na baadhi ya wakuu wa Idara pamoja Muhandisi wa Halmashauri na miradi waliyotembelea na kukagua ni pamoja na ukamilishaji wa bweni la wasichana shule ya sekondari Nyamanguta, ujenzi wa nyumba mbili za walimu (2in1) shule ya msingi Sabasita ambapo nyumba moja ya (2in1) ipo hatua ya upauaji na nyumba nyingine imeshawekwa kenchi, ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Amali iliyopo katika Kijiji cha Manchimweru na majengo yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi, majengo mengine yapo hatua ya ufungaji lenta,uwekaji kenchi, na mengine yapo hatua za ujenzi wa msingi.
Pia, walitembelea na kukagua ujenzi wa shule ya sekondari Nyaburundu, ukamilishaji wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Salama A pamoja na ukamilishaji wa matundu manne ya vyoo ambapo ujenzi upo katika hatua ya uwekaji wa milango na madirisha katika vyoo na madarasa, uwekaji wa vigaye katika vyumba vya madarasa na upigaji wa rangi.
Walitembelea na kukagua ujenzi wa shule ya msingi Nyansirori ambapo ujenzi wa majengo hayo upo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji, pia, walitembelea na kukagua ukamilishaji wa nyumba za walimu katika shule ya sekondari Mariwanda ya (2 in 1)
Walihitimisha ziara hiyo kwa kutembelea na kukagua ujenzi wa mabweni manne katika shule ya sekondari Chamriho ambapo mabweni mawili yapo hatua ya ufungaji lenta na mawili yapo hatua ya umwagaji jamvi. Pia, walitembelea na kukagua ukamilishaji wa bweni katika shule ya sekondari Hunyari.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda