Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Ndugu George S. Mbilinyi ameendelea na ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ya ujenzi iliyopo katika Jimbo la Bunda.
Kituo cha kutolea huduma za Afya, Kiloleri
Ambapo siku ya 4/5/2024 alitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kutolea huduma za Afya Kiloleri, alikagua ukamilishaji wa matundu 21 ya vyoo katika shule ya msingi Salama A, na mradi wa ujenzi wa matundu manne (4) ya vyoo katika shule ya msingi Salama A, pia alitembelea na kukagua ujenzi wa chumba kimoja cha darasa na matundu manne (4) ya vyoo katika shule ya msingi Salama Kati, ujenzi wa matundu matano (5) ya vyoo katika zahanati ya Kurusanga.
Ukaguzi wa matundu 21 ya vyoo, katika shule ya msingi Salama A
Ndugu Mbilinyi aliagiza wasimamizi wa miradi yote ya ujenzi kuhakikisha wanafuata taratibu na sheria za manunuzi ya vifaa vya ujenzi na kuhakikisha wanawasimamia mafundi vizuri ili kuharakisha kasi ya ujenzi na kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati uliopangwa.
Mkurugenzi pia, alitembelea na kukagua darasa la watoto wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Nyamuswa B na kukagua eneo la upandaji miti pamoja na uwanja ambao mwenge wa uhuru 2024 unatarajiwa kupokelewa mwanzoni mwa mwezi wa nane.
Darasa la watoto wenye mahitaji maalumu, shule ya msingi Nyamuswa B
Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji aliongozana na baadhi ya wakuu wa idara na vitengo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda