Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango (FUM) siku ya tarehe 6/5/2024 ilifanya ziara ya kutembelea na kukagua ukamilishaji wa maabara ya Kemia katika shule ya sekondari Kwiramba, ambayo imejengwa na fedha kutoka serikali kuu kwa kiasi cha Tshs Milioni 30.
Muonekano wa nje wa jengo la Maabara ya Kemia, shule ya sekondari Kwiramba
Muonekano wa ndani ya Maabara ya Kemia
Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Kwiramba Bi Ashura Ramadhani, alisema hadi sasa mradi umekamilika kwa asilimia 98.
Walimu wa shule ya sekondari Kwiramba waliishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuweza kuwapa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa maabara hiyo kwani walikuwa na upungufu mkubwa na waliomba pia, wajengewe maabara ya TEHAMA kwa ajili ya watoto kujifunza vizuri masuala ya TEHAMA kwa vitendo.
Kamati ya FUM waliagiza sehemu ya ukamilishaji wa maabara ya Kemia iliyobaki wahakikishe wanakamilisha ndani ya miezi mitatu.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda