Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango (FUM), ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ambaye ni Diwani wa Kata ya Iramba, Mh. Charles Manumbu, ilifanya ziara ya siku mbili ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda siku ya tarehe 31/10/2023 na tarehe 1/11/2023.
Kamati hiyo ilitembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa jengo la Utawala la Halmashauri, lililopo Kibara Stoo, Mradi wa maji Kibara kuelekea Mumagunga, Mradi wa kitalu cha miche kilichopo Kasahunga na Mradi wa Ujenzi wa shule ya Mkoa ya Wasichana iliyopo katika kijiji cha Bulamba, Kata ya Butimba.
Mradi wa shule ya Wasichana ya Mkoa wa Mara, uliopo Bulamba, kata ya Butimba.
Aidha, kamati ilikagua vifaa vya Mradi wa kuhimili Athari za mabadiliko ya Tabianchi (BCRAP) vilivyopo Kasahunga, vifaa hivyo ni mabomba ya maji, mabomba ya maji kwaajili ya mradi wa umwagiliaji kwenye sola, Pampu ya maji kwa ajili ya umwagiliaji katika kijiji cha Mchigondo, Mashine ya kusagia chakula cha samaki na mashine kwa ajili ya kutotoleshea vifaranga.
Ukaguzi wa mabomba ya maji yaliyopo Kasahunga
Mashine za kutotoleshea vifaranga, zilizopo Kasahunga
Kitalu cha miche, Kasahunga
Mradi wa maji uliopo Kibara.
Katika ziara hiyo, kamati iliongozana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Bw. Gervas Amata, pamoja na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda