Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imefanya ziara katika Josho la sarakwa na katika vyanzo vya mapato vya Halmashauri Novemba 10 hadi 11,2021.
Akiwasilisha taarifa fupi ya ujenzi wa Josho Mtendaji wa Kijiji cha Sarakwa Bwa. Shedrack Ezra alisema kuwa ujenzi huo umeanza 22.07.2021 na mpaka kukamilika kwa Josho hilo itagharimu kiasi cha Tsh,23,481,000.
Bwa. Ezra alibainisha chanzo cha fedha za ujenzi wa Josho hilo ni Wizara ya Uvuvi na Mifugo imetoa Tsh. 18,000,000 na Tshs.5,481,000 nguvu za wananchi wa Sarakwa.
‘Josho hili limeanza kujengwa 22.07.2021 na Inategemea kumalizika mwishoni mwa Mwezi Novemba, 2021’’Alisema Bwa.Ezra
Aidha bwa.Ezra aliongeza kusema kuwa ujenzi wa josho unaendelea kutekelezwa kwa kuzingatia sheria na taratibu zote za ujenzi,viwango stahiki vya ubora, na usalama wa mifugo.
Wakizungumza mara baada ya kupokea taarifa fupi na kukagua josho ,wajumbe wa kamati waliridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa josho hilo na kushauri kuwa mara nyingine wanapoandika andiko kwaajilii ya mradi wahakikishe kuwa mahitaji yote yanakuwepo katika andiko,kwani imebainika kuwa kuna gharama za ujenzi wa kisima kirefu kwaajili ya maji hazikuwepo katika maombi ya awali.
‘Ujenzi unaridhisha,niwapongeze Wananchi wa sarakwa kwakuendelea kujitolea katika shughuli za maendeleo’’alisema Mhe.Irobi
kamati pia ilitembea Machimbo yaliopo kijiji cha Nyaburundu kata ya Ketare ambapo ilipokea taarifa kutoka kwa kiongozi wa wachimbaji Madini Bwa. Steve Mwita kuwa Mgodi hauzalishi kutokana na mashimo kujaa maji.
Bwa.Mwita ameiomba serikali kuwawekea umeme katika eneo hilo ili uchimbaji uwendelee,kwani kwasasa wanatumia gharama kubwa katika kutoa maji kutokana hakuna umeme
"Gharama inayotumika kwasasa ni kubwa kutoa maji katika mashimo,kutokana mashine inatumia mafuta na haina nguvu ya kutoa maji ,hivyo tunaomba tuletewe umeme tufanye kazi na kuleta mapato Halmashauri "alisema Bwa.Mwita
Maeneo mengine yaliyotembelewa na kamati ni Mwalo wa Mugara,Isanju, Mugara Nyalina,Muranda na Sikiro ambapo kamati ilibaini kuwa baadhi wa wakusanyaji mapato wamekuwa si waaminifu kwakukaa na fedha muda mrefu bila kupeleka benki na wakati mwengine kutumia fedha mbichi.
Aidha kamati ilitoa agizo kwa wakusanya ushuru wote kuweka fedha zote walizonazo katika akaunti kufikia 19,November 2021.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda