Katika kuadhimisha miaka minne (4) ya Uongozi wa serikali ya awamu ya sita chini ya rais Dkt Samia Suluhu Hassan,Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh. Aswege Enock Kaminyoge, amewataka wananchi wa Wilaya ya Bunda kutoa ushirikiano wa dhati kwa viongozi ili kufikia dhamira ya serikali ya awamu ya sita katika utoaji wa huduma za jamii.
Maadhimisho hayo yamefanyika siku ya tarehe 17/03/2025 katika ukumbi wa Malaika uliopo Bunda Mji huku lengo likiwa ni kuwafamisha wananchi juu ya shughuli na mafanikio ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita katika nyanja mbalimbali.
Akizungumza wakati wa kufungua maadhimisho hayo Mh.Kaminyoge amewaagiza wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa Halmashauri na taasisi binafsi kuwatambua na kuwaheshimu viongozi wa ngazi za chini (serikali za mitaa na vijiji) ili kurahisisha utendaji kazi ikiwemo kupeleka taarifa mbalimbali kwa wananchi.
"Nawaombeni ushirikiano wa kutosha na mimi naahidi kuwapa ushirikiano unaostahili na niwakumbushe kwamba ofisi ya Mkuu wa Wilaya itakuwa wazi kusikiliza kero na changamoto za wananchi wa makundi yote na karibuni muweze kuhudimiwa"Amesema Mh Kaminyoge.
Mimi na viongozi wenzangu tunaomba ushirikiano kutoka kwenu ili kufikia adhima ya serikali ya kuhakikisha wananchi wote wanakuwa na furaha katika nchi yao, pia,ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa jitihada kubwa na utendaji kazi mkubwa katika kuhakikisha inafikia malengo makubwa ya kuwahudumia wananchi wa Tanzania ikiwemo kuhakikisha wananchi wanakuwa na amani,furaha na utulivu,kuunda tume ya haki jinai, utoaji wa msaada wa kisheria pamoja na utoaji wa huduma za kijamii na kiuchumi kwa wananchi.
Aidha,katika maadhimisho hayo, Halmashauri zote mbili pamoja na taasisi za serikali zilipata nafasi ya kuwasilisha taarifa ya matumizi ya fedha kutoka serikali kuu na wahisani kwa muda wa kipindi cha miaka minne.
Akiwasilisha taarifa ya matumizi ya fedha kwa muda wa miaka minne Afisa mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu Sai Amosi, amesema Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imefanikiwa kutekeleza shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya Elimu, ujenzi wa shule mpya za Sekondari na Msingi,kuongeza ufaulu wa wanafunzi,ulipaji wa madeni ya watumishi,upandishaji vyeo watumishi mbalimbali na uboreshaji wa sekta ya Afya.
Hata hivyo maadhimisho hayo yaliambatana na zoezi la upandaji miti katika shule ya msingi Kunzugu iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda