• Malalamiko |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Bunda District Council
Bunda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji & Ushirika
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Fedha & Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Mifugo & Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi & Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu Msingi
    • Barabara
    • Mifugo
    • Afya
    • Mazao ya kilimo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi & Mipango
      • Elimu, Afya & Maji
      • AIDS Control
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Uma
    • Video
    • Hifadhi ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAUGUZI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

Posted on: May 30th, 2025


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu Oscar J. Nchemwa, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani, ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Bunda iliazimisha siku ya tarehe 30/5/2025, katika kituo cha Afya Ikizu.


Ndugu Nchemwa aliwapongeza wauguzi wote kwa kuadhimisha siku yao Duniani, pia aliwaomba kuendelea kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia kanuni, Sheria na taratibu za taaluma zao.


" Wauguzi ni watu muhimu sana katika jamii kwani mmekuwa mkifanya kazi muhimu ya kuokoa maisha ya watu, nawapongeza sana na muendelee kuwa na moyo wa huruma wa kuendelea kuwasaidia watu wote bila ubaguzi wowote. Leo hii mmekula kiapo cha kutunza Siri na kufanya kazi kwa moyo mweupe na huruma kwa watu wote, kiapo hiki kikawe silaha yenu muhimu na mkitunze katika kuhakikisha mnatimiza majukumu yenu kwa kufanya kazi kwa weledi mkubwa huku mkizingatia kanuni, Sheria na taratibu za taaluma yenu." Alisema.



Katika risala mliyosoma Leo hii mbali na changamoto mnazokabiliana nazo, nawaomba muendelee kutimiza majukumu yenu na ninawaahidi changamoto zote nimezichukua na ninawaahidi kwenda kuzifanyia kazi kwa kuhakikisha mnakuwa na mazingira rafiki ya kufanya KAZI.


Ndugu Nchemwa alimuagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri kuhakikisha anaandaa utaratibu wa kuwapatia wauguzi mafunzo ya kuweza kuingia kwenye mfumo wa PEPMIS ili waweze kujaza majukumu yao, kuhakikisha wauguzi wote wanalipwa stahiki zao kwa wakati ili waweze kufanya kazi.


Katika maadhimisho hayo, Kaimu Mkurugenzi pamoja na wauguzi walitembelea wodi ya wazazi na kutoa zawadi kwa wamama waliolazwa wodini.



Siku ya wauguzi Duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 12/5 ya Kila mwaka.

Kwa mwaka 2025 siku ya wauguzi Duniani imebeba kauli mbiu isemayo:


" Wauguzi nguvu ya mabadiliko Duniani."

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI June 23, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI September 18, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WOTE December 20, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MAENDELEO YA UJENZI KATIKA HOSPITALI YA WILAYA

    June 27, 2025
  • BONANZA LA MICHEZO LA WATUMISHI KATI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA RORYA, BUNDA DC NA TC

    June 16, 2025
  • MRATIBU WA MRADI WA BCRAP ATAJA VIPAUMBELE VITAKAVYOENDA KUTEKLELEZWA KWA AWAMU YA PILI YA MRADI

    June 11, 2025
  • ZAIDI YA MILIONI 300 ZA POKELEWA KATIKA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUHIMILI ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI

    June 09, 2025
  • Angalia zote

Video

Mvamizi wa eneo la soko.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Baraza la Madiwani
  • Dira na Dhamira
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mpango Mkakati
  • Mpango wa Uwekezaji Sekta ya Samaki
  • Muundo wa Taasisi
  • OPRAS - Form

Viunganishi Muambata

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2023 Bundadc
  • Matokeo ya darasa la saba
  • Matokeo ya darasa la saba
  • PO-RALG
  • PO-PSM
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2019

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Kibara Stoo.

    Anuani ya Posta: 126, Bunda

    Simu: 0282621055

    Hamishika:

    Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda