Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Mwibara na Bunda Bw. Amos Kusaja amewataka wasimamizi wa Uchaguzi kwenda kufanya kazi hiyo kwa uadilifu mkuu ambapo pia amewasisitiza kuzingatia sheria na Taratibu walizoelekezwa pamoja na mafunzo ambayo wamepewa.
Ameyasema hayo wakati akifungua semina ya siku mbili ya wasimamizi hao iliyofanyika katika ukumbi wa Malaika uliopo Bunda Mji.
“Nendeni mkafanye kazi hii vyema hatumvumilia mtu ambaye atakiuka mmeapa kwa mujibu wa sheria hatutarajii kuona fujo kwenye maeneo yenu nendeni mkatumie hii elimu mliyoipata hapa kikamilifu”.
Aidha Bw. Kusaja amewakumbusha kuwa uchaguzi upo kwa mujibu wa sheria,kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali hivyo wakavizingatie kwani kwenda kinyume na hivyo watawajibika Kwa mujibu wa sheria jambo si zuri kwao.
Hata hivyo amewasihi wasimamizi hao kuepuka kuleta itikadi za vyama vyao kwa kuwa wameshakula kiapo cha kujitoa uanachama wakumbuke kuwa wapo pale kama watumishi wa Tume na si Wanasiasa.
“Kila aliyekula kiapo cha Tume atambue kuwa yeye si mwanachama wa chama chochote kuanzia sasa”amesema Kusaja.
Amewakumbusha wasimamizi hao kuwa kuzingatia muda wa kufika kituoni, ilikuepusha kuwakwamisha wananchi kukosa haki yao muhimu ya kupiga kura.
“kituo kinafunguliwa 1.00 asubuhi ni vyema kila mmoja kufika kituoni kabla ya huo muda kwaajili ya maandalizi”.amesema Kusaja
Akiongea kwa niaba ya wasimamizi wengine Linda Isinike amewasihi washiriki wengine kwenda kuwa waaminifu katika kukamilisha zoezi hilo ili likamilike kwa amani na utulivu.
Semina hii imehudhuriwa na wasimamizi 371 na wasimamizi wasaidizi 666 wa vituo vyakupiga jimbo la Mwibara na Bunda na inafanyika kwa siku mbili ambapo imehudhuriwa pia na wasimamizi ngazi ya Kata na Jimbo.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda