Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa kushirikiana na Ofisi ya rais TAMISEMI na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, wametoa mafunzo kwa viongozi wapya wa Serikali za Mitaa waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa tarehe 27 Novemba 2024. Mafunzo hayo yamefanyika siku ya tarehe 3/1/2025 katika shule ya Sekondari Mwibara.
Katika mafunzo hayo wamepata nafasi ya kupitia sheria mbalimbali zinazogusa majukumu yao ikiwemo sheria ya Serikali za mitaa sura ya 288 na 287, sheria ya fedha na sheria nyingine, pia wamehimizwa kuimarisha umoja katika utendaji kazi wao.
Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bw.George S Mbilinyi amewataka viongozi hao kuwa na maadili ya kusimamia haki za wananchi na kusimamia shughuli zote za maendeleo zinazoendeshwa katika maeneo yao.Huku akiwakumbusha kushiriki katika ukusanyajiwa mapato kwa kutoa Elimu kwa wananchi katika maeneo yao.
"Zingatieni maadili ya kazi ilikuwa viongozi bora katika maeneo yenu lakini pia hakikisheni mnasimamia vizuri mapato yote ya Kijiji na Halmashauri ili kuleta maendeleo bora katika Halmashauri yetu". Amesema Bw.Mbilinyi.
Akitoa mafunzo hayo, Mhadhiri kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa maarufu kama Hombolo Ndugu Victor Mwinyipembe kupitia somo la Uongozi na Utawala bora amesema kuwa nafasi zao za uongozi ni kwa muujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wanapaswa kufuata muongozo wa katiba katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
“Uongozi ni dhamana, mnapaswa kuwa watiifu na wanyenyekevu badala ya kuwa wenye mamlaka na madaraka na hili kuwa kiongozi bora nilazima kufuata sheria kama zinavyoelekezwa na katiba ya nchi, nilazima kuzingatia utawala bora kwa kuzingatia namna sahihi ya utumiaji wa rasilimali ili kufikia malengo". Amesema Mwinyipembe.
Kwa upande wake Mhadhiri wa chuo cha Serikali za Mitaa Ismail Juma amewataka viongozi hao kuelewa majukumu yao ili kuepuka kufanya majukumu ya watu wengine na kuwahamasisha zaidi kufanya vikao vya mara kwa mara katika vijiji vyao pamoja na kuwashirikisha wananchi na wataalamu katika maamuzi yeyote ya kimaendeleo ili kuepuka kuleta migogoro.
Hatahivyo mada zilizofundishwa zilihusu sheria, uongozi bora, usimamizi wa fedha, mipango ya maendeleo na udhibiti wa ardhi. Pia viongozi hao walitoa ahadi ya kusimamia haki na kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda