Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bi. Changwa M. Mkwazu siku ya tarehe 1/11/2023 alikutana na Wadau kutoka Shirika la uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) na kufanya mkutano mdogo na wananchi wa eneo la Kibara.
Lengo la mkutano huo ni kuwaeleza wananchi fursa itakayopatikana kutokana na uwekezaji unaotarajiwa kufanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda hasa katika kijiji cha Kibara eneo la Mwaloni.
Mdau kutoka TASAC Kapteni Emmanuel Marijani alisema, wanatarajia kujenga kiwanda cha kuchakata Samaki na Dagaa, pamoja na kuwajengea kituo cha uokoaji na utafutaji katika eneo hilo la Mwaloni, na ujenzi huo unatarajiwa kuanza mapema Januari, 2024.
Kapteni Marijani alisema, tunataka tuipe Halmashauri uwezo wa kukusanya mapato kwa wingi na Wananchi wake kuweza kujipatia fursa mbalimbali ikiwemo kujiongezea mapato sababu shughuli za biashara zitafunguka kwa wingi kutokana na muingiliano wa watu mbalimbali kufika mahali hapa.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda B. Changwa M. Kwazu, aliwashukuru Wadau hao kwa kuwaletea fursa hiyo katika Halmashauri, kwani kutokana na Ujenzi huo kutasadia kukuza uchumi.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mh. Dr. Vicent Anney aliwashukuru Wadau kwa kuchagua kuja kuwekeza mahali hapa, pia, aliwashauri kuwa na andiko la mradi ambalo linaonyesha umri wa mradi kuanzia kuanza kwake hadi ukamilishaji wake na kuwataka kuunda kamati maalumu ambayo ndio itakayokuwa inasimamia mradi mzima na kuhakikisha wanashrikiana kwa pamoja kuanzia kwenye Halmashauri hadi Wilayani maana ndio walengwa wakuu wa mradi huu.
Mradi huu unafadhiliwa na Bank ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) wakishirikiana na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda