• Malalamiko |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Bunda District Council
Bunda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji & Ushirika
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Fedha & Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Mifugo & Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi & Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu Msingi
    • Barabara
    • Mifugo
    • Afya
    • Mazao ya kilimo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi & Mipango
      • Elimu, Afya & Maji
      • AIDS Control
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Uma
    • Video
    • Hifadhi ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Siku ya Wazee Duniani yaadhimishwa Wilayani Bunda

Posted on: October 24th, 2017

Siku ya Wazee Duniani imeadhimishwa Wilayani Bunda katika Kijiji cha Neruma, Kata ya Neruma ambapo Wazee mbalimbali walipata fursa ya kukutana, kuburudika pamoja, kupata ujumbe uliobebwa na maadhimisho hayo na hatimaye kupokea vitambulisho vya matibabu bure kwa Wazee. Siku hii Duniani huadhimishwa tarehe 1/10/2017, wilayani Bunda siku hii iliadhimishwa tarehe 20/10/2017 ambapo mgeni rasmi alitakiwa kuwa Ndg. Lydia Bupilipili ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda lakini kutokana na kuwa na majukumu mengine aliwakilishwa na Katibu Tawala Wilaya Ndg. Masalu Kisasila.

Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ilikuwa ni: "Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Tuthamini Mchango, Uzoefu na Ushiriki wa Wazee kwa Maendeleo ya Taifa".

Pamoja na mambo mengine, tukio muhimu kwenye maadhimisho hayo lilikuwa ni kuwakabidhi Wazee wapatao 235 vitambulisho vya matibabu bure. Lengo la Idara za Afya na Maendeleo/Ustawi wa Jamii ni kutoa jumla ya vitambulisho kwa Wazee 9,994 ifikapo Mwaka 2020.

Pia, mgeni rasmi aliyeongozana na Viongozi wengine akiwemo Mkurugenzi Mtendaji (W) Ndg. Amos Kusaja, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Mhe. Isack Maela alitumia fursa hiyo kutoa msisitizo wa Idara ya Afya kutenga Dirisha maalumu katika Vituo vya kutolea huduma za afya zikiwemo Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati ili kuboresha utoaji huduma kwa Wazee hao. Wauguzi nao walitakiwa kutumia lugha nzuri pale wanapowahudumia Wazee ambapo Wazee nao waliaswa kuendelea kuwa washauri wazuri wa Vijana ili kunusuru maadili ya Vijana na jamii kwa ujumla.


Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI KWA NAFASI ZA UDEREVA May 07, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI September 18, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WOTE December 20, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ROJECT ZAWADI YAIPIGA TAFU MASHINDANO YA UMITASHUMTA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA

    April 07, 2025
  • WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WAPEWA TUZO NA ZAWADI .

    April 03, 2025
  • TIMU YA WATAALAMU WA TATHIMINI NA UFUATILIAJI WA MIRADI YA MAENDELEO WAFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI

    March 27, 2025
  • MKUU WA WILAYA ATETA NA VIONGOZI WA HALMASHAURI NA WA TAASISI

    March 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Mvamizi wa eneo la soko.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Baraza la Madiwani
  • Dira na Dhamira
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mpango Mkakati
  • Mpango wa Uwekezaji Sekta ya Samaki
  • Muundo wa Taasisi
  • OPRAS - Form

Viunganishi Muambata

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2023 Bundadc
  • Matokeo ya darasa la saba
  • Matokeo ya darasa la saba
  • PO-RALG
  • PO-PSM
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2019

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Kibara Stoo.

    Anuani ya Posta: 126, Bunda

    Simu: 0282621055

    Hamishika: 0742163056

    Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda