"Shirika la Rafiki SDO ni mradi unaoshughulika na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na lengo kuu la mradi ni kutokomeza hali ya ukatili wa kijinsia na kwa Mkoa wa Mara wapo Halmashauri Saba". Amesema Ndugu Ramadhan Luheja Nyanda.
Ndugu Nyanda amesema katika Mkoa wa Mara wamekuwa wakishirikiana na serikali katika kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, kwa kuwasaidia kuwapeleka chuo cha Veta kwa ajili ya kujifunza ufundi wa ushonaji nguo na ufundi mwingine, ambapo baada ya kuhitimu wamekuwa wakiwawezesha mashine pamoja na vifaa vya kuanzia kazi, ili kujiendeleza kiuchumi.
Ramadhan Luheja Nyanda ni Afisa Afya na UKIMWI kutoka shirika la Rafiki SDO, aliyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyoadhimishwa siku ya tarehe 1/12/2024 katika stendi ya mabasi Nyamuswa iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Shirika la Rafiki SDO lilimkabidhi Bi. KIHENGU JUMA, Mtoto anayeishi katika mazingira magumu katika Kata ya Nyamuswa, ambapo kupitia shirika Hilo ameweza kusomeshwa mafunzo ya ufundi wa ushonaji nguo katika chuo cha ufundi Veta na kukabidhiwa mashine ya Cherehani pamoja na vifaa vya ushonaji na majora mawili kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi.
Naye, KIHENGU JUMA mnufaika wa shirika la Rafiki SDO amewashukuru wadau wa shirika kwa msaada walioutoa kwa kumpatia mafunzo na kumuwezesha kupata mashine na vifaa vya ushonaji, amewashauri mabinti wenzake wanaotoka katika mazingira magumu kama yeye kutokukata tamaa ya maisha Bali waendelee kumuamini Mungu na kusimamia ndoto zao.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda