Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mh. Alexander Mnyeti amesema, serikali ya Awamu ya sita ya Mh. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetenga kiasi cha Tshs Millioni 400 kwa ajili ya kuchanja na kuogesha mifugo nchi nzima na tayari Zaidi ya Tshs Million 30 zimeshatoka kwa ajili ya kuanza kwa zoezi hilo.
Mh. Mnyeti aliyasema hayo wakati wa hafla fupi ya ugawaji wa madume 20 ya Ng’ombe yaliyoboreshwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda siku ya tarehe 27/9/2024 , katika kijiji cha Mariwanda kilichopo Kata ya Hunyari.
“Lengo la kugawa Ng’ombe hizi ni ili wafugaji wote muachane na ufugaji wa kizamani muanze kufuga kisasa, Mh. Rais ametuagiza mimim na Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha tunazigawa Ng’ombe hizi katika Halmashauri zote nchini kwa ajili ya kuleta matokeo chanya na yenye tija katika ufugaji wa kisasa kwa kupata thamani ya mifugo yetu.” Alisema Mh. Mnyeti.
Naibu Waziri alisema, sababu ya Mh. Rais kuamua kugawa madume haya ni ili wafugaji waachane na ufugaji wa kizamani unaomfanya mfugaji kumiliki Ng’ombe wengi wenye gharama ndogo. Kumbe unaweza kufuga Ng’ombe wachache wenye thamani kubwa na ukapata faida Zaidi.
“Tuingie kwenye ufugaji wa kisasa kwa kuwabadilisha Ng’ombe tulionao kwa kuwapandikiza na Ng’ombe hawa walioboreshwa ili Ndama watakaozaliwa wazaliwe chotara. Ng’ombe wadogowadogo hawa na waliokondeana hawana faida wala tija kwa mfugaji.” Alisema Naibu Waziri.
Mh. Mnyeti alisema niwapongeze kwa ushirikiano mzuri na mkubwa mlionao hapa kuanzia kwa Mh. Mbunge Mwenyekiti wa chama cha wafugaji taifa na wafugaji wote, naombeni mpokee Ng’ombe hawa na niwahakikishie tutawaongezea madume wengine 20 na kupafanya mahali hapa kuwa shamba darasa kwa ajili ya kuja wengine kujifunza.
Naibu Waziri alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda Bw. George S. Mbilinyi kuhakikisha anafanya utafiti wa kutosha wa mahali hapa na kuongeza idadi ya vikundi vya wafugaji ili wengine waweze kuja katika Halmashauri hii kujifunza.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda