Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa, Ndugu Ismail Ussi, siku ya tarehe 23/8/2025 alizindua miradi mbalimbali ya Maendeleo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Ndugu Ussi, alizindua nyumba za walimu zilizopo katika shule ya msingi SABASITA, ambazo zimejengwa kwa fedha za serikali, nyumba hizo ni (2 in 1), mara mbili, ambapo familia nne zinaishi pamoja, Ndugu Ussi alimshukuru Mh. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha ujenzi wa nyumba hizo kwa wakati Mmoja katika shule hiyo ya msingi.
Alimpongeza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, kwa kupata nafasi hiyo ya upendeleo wa kujengewa nyumba nyingi za watumishi katika shule ya msingi SABASITA, lengo likiwa kuboresha malazi ya watumishi wanaoishi mbali na maeneo ya shule, na pia kusaidia kuboresha elimu katika shule ya msingi SABASITA.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, pia, alizindua klabu ya wapinga rushwa katika shule ya msingi SABASITA, ambapo aliwapongeza wanafunzi kwa kutunga mashairi mazuri yanayoelezea kupinga rushwa katika jamii
na kuwaasa wananchi kuacha kupokea rushwa hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika mwezi Kumi, 2025. Aliwashauri wananchi wote kuhakikisha wanaenda kupiga kura ili waweze kuchagua viongozi sahihi ambao watashirikiana kwa pamoja katika kuleta maendeleo.
Aidha, Ndugu Ussi alikagua na kuzindua daraja la Chingurubila ambapo linaenda kusaidia wananchi wengi waishio katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda hasa katika Kata ya Namuhula na maeneo jirani kuweza kupita kwa urahisi na uhakika katika kipindi chote cha mwaka, hivyo kuzinduliwa kwa daraja kutasaidia kurahisha shughuli za kiuchumi na kimaendeleo kwa wananchi wote wa kata ya Namuhula na maeneo ya jirani.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, amezindua mradi wa maji Kabainja, uliopo kata ya Kasuguti katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, ambapo kuzinduliwa kwa mradi huo, kunaenda kupunguza kero ya maji kwa wananchi wa kata ya Kasuguti na maeneo ya jirani.
MWENGE wa uhuru, 2025:
"Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu, 2025 kwa Amani na Utulivu."
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika:
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda