Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda Ndugu. George S. Mbilinyi siku ya tarehe 22/2/2025 aliendelea na ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa upande wa jimbo la Mwibara.
Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji aliambatana na wakuu wa idara ya elimu Msingi na Sekondari, Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri, pamoja na Mhandisi wa Halmashauri katika kutembelea na kukagua miradi hiyo ya ujenzi inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Bunda kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Mkurugenzi, pamoja na timu yake, walitembelea na kukagua ukamilishaji wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Namibu A pamoja ujenzi wa matundu 6 ya vyoo, ambapo ujenzi wake upo katika hatua ya ukamilishaji.
Pia, walitembelea na kukagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ya awali na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Bulomba, ambapo ujenzi wake upo katika hatua ya upigaji lipu katika vyumba hivyo vya madarasa, na vyoo vipo hatua ya upauaji. Pia, walikagua ujenzi wa madarasa mawili ya msingi ambapo yapo hatua ya upigaji wa lipu, na walikagua ujenzi wa matundu 6 ya vyoo ambapo ujenzi wake upo katika hatua boma.
Ukamilishaji wa matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Igundu
Ukamilishaji wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Igundu
Walitembelea na kukagua ukamilishaji wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Igundu, pia, walitembelea na kukagua ujenzi wa shule ya sekondari ya Amali iiyopo Kijiji cha Makwa kata ya Nampindi ambapo ujenzi upo katika hatua mbalimbali za upauaji wa baadhi ya majengo, upigaji wa lipu, na ujenz wa vyoo ambao upo katika hatua ya ujenzi wa boma.
Pia, walitembelea na kukagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari ambayo ipo Kijiji cha Mayolo, kata ya Mahyolo ambapo pia ujenzi umefikia hatua mbalimbali za ukamilishaji kwa baadhi ya majengo ambayo yapo katika hatua ya upauaji, uwekaji wa milango katika vyumba vya madarasa na ofisi, pamoja ujenzi wa maabara za fizikia, biolojia na kemia.
Aidha, Mkurugenzi alitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mabweni manne ya wasichana, nyumba za walimu, na madarasa pamoja na bwalo la shule ambapo ujenzi wa majengo hayo upo katika hatua mbalimbali zikiwemo upigaji wa lipu, na ufungaji wa lenta kwenye baadhi ya mabweni.
Mkurugenzi alikamilisha ziara yake kwa kutembelea na kukagua ukamilishaji wa kituo cha Afya Isanju ambapo mafundi wapo katika hatua za ukamilishaji wa majengo mbalimbali katika kituo hicho cha Afya, na pia alikagua eneo la ujenzi wa nyumba mpya za watumishi katika kituo, pia alitembelea na kukagua ujenzi wa zahanati inayojengwa ka fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ambayo ipo katika Kijiji cha Nyamitwebili.
Mkurugenzi Mtendaji aliwaagiza wasimamizi wa miradi yote hiyo kuhakikisha wanawasimamia mafundi ili waweze kuongeza kasi katika kuhakikisha wanaikamilisha na kuikabidhi mapema ili ianze kutumika kama inavyotakiwa, pia aliwaagiza kuhakikisha wanawahimiza wazabuni wote wanaotakiwa kuleta vifaa katika miradi wanavileta mapema ili kuzuia kukwamisha na kuchelewesha ukamilishaji wa miradi.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda