Ili kuendeleza usalama wa dunia na kizazi kijacho tunahitaji kuchukua hatua za haraka ili kupunguza kiwango cha hewa ukaa(kaboni) katika mazingira yetu.Unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni suluhisho mojawapo ambalo linahitaji ushiriki mkubwa wa sekta mbalimbali ili kutatua changamoto za kiafya na kimazingira.
Hayo yamesememwa Leo na Mkuu wa Wilaya ya Mhe Lydia Bupilipili wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji katika Halmshauri ya Wilaya ya Bunda.
“Wiki hii ya unyonyeshaji inaeleza uhusiano uliopo kati ya unyonyeshaji watoto maziwa ya mama na afya bora pamoja na kulinda mazingira yetu kama kauli mbiu inavyoeleza”.
Mhe Bupilipili amesema kuwa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni fursa muhimu ya kutoa hamasa kwa jamii katika kulinda,kuimarisha na kuendeleza unyonyeshaji.
“Ni muhimu kwa kila mzazi kuzingatia maelekezo ya Watalaam wa afya pindi anaposhika mimba mpaka anapojifungua ikiwa na pamoja na ukuzaji wa mtoto”.
Aidha, amesema watoto wanapotimiza miezi sita waanzishiwe vyakula vya nyongeza vyenye ubora katika lishe huku wakiendelea kunyonyeshwa hadi watakapotimiza umri wa miaka miwili.
Kwa upande wa takwimu kwa Halmashauri ya Wilaya Bunda hali ya unyonyeshaji inaonesha kuwa watoto wanaoanzishiwa maziwa ya mama wakati wa kuzaliwa ni asilimia 94 na wanaoendelea na kunyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kupewa chochote hata maji ni asilimia 20 tu.
“Tafsi yake ni kuwa kati ya watoo 100 watoto 20 wananyonya maziwa ya mama pekee bila kupewa chochote hadi kufikia umri wa miezi sita”.amesema
Naye,Mganga Mkuu wa Halmashauri Dkt Nuru Yunge amesema Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani kwa mwaka 2020 yamebebwa na kauli mbiu inayosema“Tuwawezeshe Wanawake kunyonyesha Watoto kwa Afya bora na ulinzi wa Mazingira”.
Dkt Yunge amesema kuwa unapojifungua katika kituo cha kutolea huduma,l huduma zinaanza pale pale ikiwemo ushauri wa unyonyeshaji huzurio la kwanza kabla ya miezi mitatu kwa wamama wajawazito kila unapohudhuria kliniki unapata huduma ya ushauri ikiwemo jinsi yakulea mtoto pindi utakapo jifungua.
“Mtoto si wako pekeako mtoto ni wataifa”.
Aidha Dkt Yunge alitoa rai kwa wakina mama kunyonyesha watoto maziwa ya mama pekee kwa miezi sita baada ya miezi sita mtoto anaeza kuchanganyiwaa vyakula vyengine.
Siku 1000 ni muhimu sana kwa maisha ya mtoto tangu mimba inatungwa pamoja na unyonyeshaji unaingia katika hizi siku, Madhara ya kutomnyonyesha vizuri mtoto ni makubwa hayatibiki, hivyo kila mzazi azingatie maelekezo ya wataalamu ili watoto wakue katika mazingira bora pamoja na kuwa na afya imara.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda