Zaidi ya vijana 570 waliohitimu mafunzo ya mgambo katika wilaya ya Bunda amepatiwa ajira katika kampuni ya ulinzi ya SUMA JKT.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa wilaya hiyo Mwalimu Lydia Bupilipili ambapo amesema kuwa asilimia kubwa ya vijana waliohitimu mafunzo ya mgambo walikosa ajira na kujiingiza katika ujangiri ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti na uvuvi haramu ndani ya ziwa Victoria.
"Hivi karibuni tulitembelea magereza na kukuta asilimia 80 ya vijana kati ya umri wa miaka 20 hadi 45 wanakabiliwa na kesi za ujangiri na uvuvi haramu na wengi wao wamepitia mafunzo ya mgambo baada ya kukosa ajira wakajiingiza katika shughuli hizi kwa kurisishwa na ndugu au wazazi wao." amesema Bupilipili.
Kutokana na vijana wengi kujihusisha na ujangiri na uvuvi haramu, wilaya ya Bunda alianda mpango maalumu wa kutoa ajira kwa vijana waliomaliza mafunzo ya mgambo, huku wengine wakipatiwa mafunzo mbalimbali katika Chuo cha ufundi Kisangwa jambo ambalo litasaidia kumaliza ujangili na uvuvi haramu kwa vijana kupata ajira na kujiajiri wenyewe kupitia mafunzo na Elimu tunazo wapatia juu zinzojitokeza.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda