Mkuu wa Mkoa wa Mara Mh Adam Malima amefanya ziara katika halmashauri ya Wilaya ya Bunda na kukagua ujenzi wa barabara inayoanzia Bulamba mpaka Kisorya.
Ambapo alimsisitiza Mkandarasi kukamilisha ujenzi wa barabara hyo kwa haraka kufikia Aprili 2020.
Aidha Mkuu wa Mkoa alitembelea kituo cha afya Kisorya na kukagua majengo mapya ya kituo hicho ambapo inaonesha kukamilika kwa asilimia tisini na tisa yamekamilika. Pamoja na mambo mengine alibaini kutokuwepo kwa umeme katika baadhi ya majengo na maji ya uhakika hasa katika jengo la wazazi.Hivyo alitoa agizo kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Bunda kuhakikisha huduma hizo zinapatikana haraka iwezekanavyo kwani Kuna baadhi ya majengo hayajaanza kutumika kwa sababu ya changamoto ya ukosekanaji wa huduma hizo.
Mkuu wa Mkoa alitembelea Makao Makuu mapya ya halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambayo yamehamia rasmi katika ya Kata ya Kibara, ofisi za Tarafa ya Nansimo tarehe 24/10/2019 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mh Rais kuwa kila halmashauri ihamie katika eneo lake la kiutawala. Aidha mkuu wa Mkoa alikagua ofisi katika Makao Makuu mapya ya Halmashauri ya Wilaya Bunda na kukutana na Changamoto ya baadhi ya majengo kutokua na umeme hivyo akamuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda kutatua changamoto hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa vyumba vyote vya ofisi za Makao Makuu zinakua na vitendea kazi muhimu vitakavyo wawezesha Watumishi kutoa huduma kwa wananchi.
Mwisho Mkuu wa Mkoa aliongea na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Bunda na kuwagiza watumishi wote wahakikishe kuwa wamehamisha huduma kutoka Makao Makuu ya zamani kwenda Makao Makuu mapya.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda