Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Bi Changwa M. Mkwazu alimkaribisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Mh. Charles Manumba kufungua Baraza la Kata lililofanyika siku ya tarehe 13/11/2023, katika ukumbi wa Halmashauri, uliopo Kata ya Kibara Stoo.
Mwenyekiti wa Baraza la Kata, Mh. Charles Manumbu aliwakaribisha Waheshimiwa Madiwani pamoja na Watumishi wote wa Halmashauri waliohudhuria katika mkutano huo wa Baraza la Kata kwa Robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Mh. Manumbu alisema, lengo la mkutano huu, ni kupokea taarifa mbalimbali kutoka katika kila Kata na kuzijadili kwa pamoja, hivyo Waheshimiwa Madiwani waliweza kuwasilisha taarifa zao.
Aidha, Mwenyekiti wa Baraza alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha anasimamia suala la ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vyote kwa usahihi, hasa kwa upande wa Samaki na Dagaa, pamoja na vyanzo vingine vya mapato.
“Tunapoenda kwenye ziara Wakuu wote wa Idara na Vitengo lazima wawepo na hakuna kukaimisha pasipo kuwa na ruhusa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji”.Alisema Mh. Manumbu.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda