Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bunda Bi. Changwa M. Mkwazu siku ya tarehe 28/9/2023 alifunga mafunzo kwa Watendaji wa Vijiji na kata yaliyofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki lililopo Kibara.
Mafunzo hayo yalilenga kuwafundisha namna ya kutumia mfumo wa ulipaji na matumizi ya fedha za serikali katika vituo vya kutolea huduma.
Bi. Mkwazu alisema ni muhimu kuendelea kujifunza mfumo huu sababu hili ni agizo kutoka serikali kuu ya kutaka kutumia mfumo katika matumizi ya ulipaji wa fedha kutoka katika Kata na vijiji. Kikubwa itatusaidia kutuondolea usumbufu wa kuchelewa kufunga mahesabu yetu kwa mwaka, kila mmoja aende akapambane katika kufanya kazi kwa bidi ili tuweze kupata hati iliyo safi.
“Tunao uwezo wa kufanya kazi kwa bidii, niwaombe muende mkapambane na tuendelee kupeana taarifa huko kutoka katika Kata na Vijiji vyenu, ili tuweze kuzitatuta changamoto mnazo kabiliana nazo kwa pamoja. Wale ambao hamsomi mapato na matumizi kwa wananchi wenu, mjitahidi kuwasomea wanakijiji mapato na matumizi maana ni haki yao.” Alisema Bi. Mkwazu.
Mkurugenzi mtendaji aliwaomba, Watendaji wa Kata na Vijiji walete takwimu zilizo sahihi za vyanzo vyao vya mapato na mahali sahihi vilipo, pia aliwaagiza waende wakasimamie masuala ya usafi wa uchimbaji wa vyoo vilivyo bora sababu kuna mlipuko wa ugonjwa wa kuhara na tapika katika mkoa wetu.
Alisema, mwaka huu kuna uwezekano wa kuwa na mvua za Elnino, hivyo aliwaagiza kwenda kusimamia katika kusafisha mitaro huko katika mitaa wanayoishi kwa ajili ya kuepusha kuziba kwa mitaro na kupelekea milipuko ya magonjwa mbalimbali ya kutuama kwa maji machafu kipindi cha mvua.
Naye, Afisa hesabu wa halmashauri Bw. Jacob Jeconia alimwambia Mkurugenzi mtendaji mafunzo haya yamelenga matumizi sahihi ya mapato serikalini hivyo aliwaagiza Watendaji wa Kata na Vijiji wasifanye kazi nje ya mfumo huu katika manunuzi na matumizi yoyote ya ulipaji wa fedha za serikali.
“Mfumo huu umerahisisha sana katika manunuzi na namna ya kupata wazabuni mbalimbali na namna ya kuwalipa kupitia mfumo huu. Pia utawasaidia katika kuweka hesabu zao sawa na kuwapatanisha na Bank na kuwarahisishia kufunga hesabu zao za kila mwezi na kwa mwaka, pasipo kwenda Bank mara kwa mara kufuata taarifa”. Alisema Bw. Jeconia.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda