• Malalamiko |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Bunda District Council
Bunda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji & Ushirika
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Fedha & Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Mifugo & Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi & Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu Msingi
    • Barabara
    • Mifugo
    • Afya
    • Mazao ya kilimo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi & Mipango
      • Elimu, Afya & Maji
      • AIDS Control
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Uma
    • Video
    • Hifadhi ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mkakati wa kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi kunufaisha wanabunda dc

Posted on: December 25th, 2019

KATIKA kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ikiwemo ukame unaosababisha upungufu wa chakula, Halmashauri ya Wilaya ya Bunda inakusudia kuanzisha mradi mkubwa wa kukabiliana na hali hiyo.

Mradi huo utakuwa na maeneo mbalimbali ikiwemo ufugaji wa samaki, kilimo cha kisasa cha mpunga, uboreshaji wa kilimo cha muhogo na alizeti na upandaji miti.

Akizungumza baada ya kutembelea maeneo yanayokusudiwa kutekelezwa mradi huo akiongozana na maofisa kutoka Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Ofisi ya Makamu wa Rais,afisa Mipango wa Halmashauri ya Bunda ambae pia Mratibu wa mradi huo, Dickson Balige  alisema utakapokamilika utatoa faida mbalimbali ikiwemo uhakika wa chakula na faida za kiuchumi.

Balige alisema mradi huo umegawanyika katika sehemu nne ambazo ni ufugaji wa samaki wa vizimba na mabwawa, kilimo cha mpunga na mazao ya bustani, ambacho hakitatumia dawa.

Pia, alisema mradi huo utahusisha uboreshaji wa kilimo cha muhogo na alizeti na kwa upande wa mazingira kutakua na upandaji wa miti na uhifadhi wa vilima vipara  na ufugaji wa nyuki.

Aidha, alisema kupitia mradi huo kutachimbwa visima virefu vya maji ambavyo pia vitanufaisha wananchi wanaozunguuka maeneo ya mradi.

“Mradi huu utachimba visima virefu na utafufua mradi wa maji ambao ulisimama kwa  muda mrefu katika Kijiji Cha Isanju na Kasahunga. Tunataka njaa iishe kwa maeneo yote yatakayonufaika," alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya Bunda, Amos Kusaja alisema mradi huo utasaidia kuinua uchumi wa wanavijiji watakao vifikiwa na kuongeza mapato ya wilaya.

Alitoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili mradi huo uweze kufanikiwa.

Kwa upande wake Mratibu wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi kutoka NEMC, Fredrick Mulinda, alisema wametembelea maeneo yanayokusudiwa kujengwa mradi huo na kuridhika nayo kwa kuwa yanaendana na shughuli hiyo.

“Mradi huu utaleta manufaa kwa wananchi na kupunguza hali ya umasikini kwa wakazi wa vijijini Bunda unaochangiwa pia na mabadiliko ya tabianchi,” alisema.


MATUMAINI YA WENGI

Nyariho Chibara mkazi wa Kijiji cha Isanju, alisema endapo mradi huo utakamilika utakuwa na manufaa kwao kwa namna mbalimbali ikiwemo kutengeneza fursa ya kujipatia kipato.

“Tunaweza kuutumia kama chuo hasa kwa upande wa kilimo na ufugaji kisha na sisi kwenda kutekeleza miradi yetu kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja,” alisema.

Janeti Paskali mkazi  wa kijiji hicho alisema tatizo la upungufu wa chakula mara nyingi huwaathiri wanawake ambao ndio huishi muda mrefu na watoto na wanafamilia wengine wasio na uwezo wa kujitafutia, hivyo kupatikana kwa mradi utakaotoa uhakika wa chakula ni jambo la kushukuru.

Mradi huo unaotarajiwa kuanza utekelezwaji hivi karibuni utaghalimu sh. bilioni 3.2kwa udhamini wa Mfuko wa Maziangira Duniani.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI KWA NAFASI ZA UDEREVA May 07, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI September 18, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WOTE December 20, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ELIMU IENDELEE KUTOLEWA KWA VIJANA RIKA BALEHE.

    May 31, 2025
  • WAUGUZI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

    May 30, 2025
  • ELIMU IENDELEE KUTOLEWA KWA WANUFAIKA WA MRADI WA BCRAP

    May 15, 2025
  • VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYATEMBELEWA NA KUKAGULIWA NA KAMATI YA MIKOPO NGAZI YA HALMASHAURI

    April 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Mvamizi wa eneo la soko.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Baraza la Madiwani
  • Dira na Dhamira
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mpango Mkakati
  • Mpango wa Uwekezaji Sekta ya Samaki
  • Muundo wa Taasisi
  • OPRAS - Form

Viunganishi Muambata

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2023 Bundadc
  • Matokeo ya darasa la saba
  • Matokeo ya darasa la saba
  • PO-RALG
  • PO-PSM
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2019

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Kibara Stoo.

    Anuani ya Posta: 126, Bunda

    Simu: 0282621055

    Hamishika:

    Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda