• Malalamiko |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Bunda District Council
Bunda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji & Ushirika
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Fedha & Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Mifugo & Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi & Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu Msingi
    • Barabara
    • Mifugo
    • Afya
    • Mazao ya kilimo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi & Mipango
      • Elimu, Afya & Maji
      • AIDS Control
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Uma
    • Video
    • Hifadhi ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MIRADI YA VYOO NA MATANKI YA KUVUNIA MAJI YANZINDULIWA WILAYANI BUNDA

Posted on: December 7th, 2017

Mkuu wa  Wilaya ya Bunda Mhe. Lydia Bupilipili amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Kigoma Malima katika uzinduzi wa  miradi ya vyoo na matanki ya kuvunia maji ya mvua  katika halmashauri ya Wilaya ya Bunda. Miradi hiyo imefadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la PCI – Tanzania chini ya ufadhili wa Serikali ya Marekani kupitia Wizara ya Kilimo ya Marekani (USDA).  Uzinduzi wa miradi hiyo iliyopo katika Kata 3 za Mugeta, Salama na Ketare  umefanyika katika Shule ya Msingi Sanzate iliyopo katika Kata ya Mugeta. Katika  uzinduzi huo jumla ya vyoo 6 na matanki 9 ya kuvunia maji yamezinduliwa. Miradi hiyo yenye jumla ya thamani ya Tshs   330,259,576.19 itawanufaisha wanafunzi 7,532 pamoja na walimu 118. Shule za msingi zilizonufaika na mradi  huo ni pamoja na Sanzate, Rakana, Tingirima, Salama Kati, Salama ‘A’,  Kurusanga, Nyang’aranga,  Masaba, Nyaburundu na Kambarage.

Pamoja na ufadhili wa miradi hiyo, shirika la PCI – Tanzania pia limechamgia jumla ya  mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo ya msingi sanzate ikiwa ni kutambua jitihada zinazofanywa na uongozi na pia jamii kwa ujumla katika usimamizi mzuri wa miradi inayotekelezwa shuleni hapo. Akipokea mifuko hiyo ya saruji, Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Lydia Bupilipili aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa, aliwahamasisha wananchi kushiriki katik kuchamgia shughuli za maendeleo ya Elimu ambapo aliweza kuchangisha jumla ya mifuko mingine 100 ya saruji kutoka kwa wananchi waliohudhuria na pia viongozi wa Serikali waliohudhuria uzinduzi huo.

 Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Bunda kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara pia aliwaagiza wananchi wote kuhakikisha kunakuwepo na hali ya uendelevu wa miradi yote inayotekelezwa na shirika hilo la PCI – Tanzania ikiwa ni pamoja na mradi wa utoaji wa chakula kwa wanafuzi mara baada ya muda wa wafadhili hao kufikia kikomo. Pia aliwataka viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Sanzate kuhakikisha wanasimamia kikamilifu shughuli zote za maendeleo zinazotekelezwa katika kijiji hicho.

Akihitimisha hotuba yake Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Lydia Bupilipili kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Wa Mara Mhe. Adam Kigoma Malima aliushukuru uongozi wa shirika la PCI  Tanzania pamoja na walipa kodi wa Marekani kupitia Wizara ya Kilimo (USAID) kwa msaada mkubwa wanaotoa kwa wananchi wa Bunda ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali yetu katika kuwaletea  maendeleo wananchi wa Bunda  chini ya uongozi wa Rais wetu Mhe. John Pombe Magufuli.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI KWA NAFASI ZA UDEREVA May 07, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI September 18, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI WOTE December 20, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ELIMU IENDELEE KUTOLEWA KWA VIJANA RIKA BALEHE.

    May 31, 2025
  • WAUGUZI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

    May 30, 2025
  • ELIMU IENDELEE KUTOLEWA KWA WANUFAIKA WA MRADI WA BCRAP

    May 15, 2025
  • VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYATEMBELEWA NA KUKAGULIWA NA KAMATI YA MIKOPO NGAZI YA HALMASHAURI

    April 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Mvamizi wa eneo la soko.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Baraza la Madiwani
  • Dira na Dhamira
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mpango Mkakati
  • Mpango wa Uwekezaji Sekta ya Samaki
  • Muundo wa Taasisi
  • OPRAS - Form

Viunganishi Muambata

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2023 Bundadc
  • Matokeo ya darasa la saba
  • Matokeo ya darasa la saba
  • PO-RALG
  • PO-PSM
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2019

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Kibara Stoo.

    Anuani ya Posta: 126, Bunda

    Simu: 0282621055

    Hamishika:

    Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda