Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Samia Suluhu Hassan amehutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Kitaifa, Butiama Mkoani Mara.
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ilikuwa miongoni mwa Halmashuari Tisa (9) za Mkoa wa Mara zilizoshiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo.
Makamu wa Rais katika kilele hicho alipata wasaa wa kuzungumza na Wananchi huku akitilia mkazo suala la utunzaji mazingira na kusema kuwa tusipotunza mazingira, mazingira yana tabia ya kutuadhibu na adhabu hiyo huwa endelevu.
Mbali na Makamu wa Rais, wengine waliohudhuria maadhimisho hayo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi, Mke wa Mwl. Nyerere Mama Maria Nyerere, Viongozi Mbalimbali wa Serikali, Wanaharakati wa kutunza mazingira na Wananchi toka maeneo mbalimbali.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda