Wilaya ya Bunda imeadhimisha sherehe za maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara, siku ya tarehe 9/12/2024,zilizofanyika katika ukumbi wa Malaika uliopo Bunda Mjini.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda Ndugu,Salum Khalfani Mtelela akiwa ni mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh. Dkt Vicent Anney.
Katika maadhimisho hayo wageni mbalimbali walialikwa na mada mbalimbali ziliwasilishwa na watoa mada kutoka sehemu tofauti, ambapo katika mada hizo ziligusa maendeleo ya vijana katika masuala ya uwekezaji kiuchumi na kiteknolojia, ambapo wananchi waliweza kuzijadili kwa pamoja.
Katika kongamano hilo mchokoza mada Mwalimu Kabeo alisema, wananchi wanatakiwa washirikishwe kwenye masuala ya kiuchumi ili wapate kujua fursa mbalimbali na waweze kushiriki katika fursa hizo.
Pia, wananchi wanatakiwa wawezeshwe maeneo ya uwekezaji ili waweze kufanya biashara mbalimbali kwaajili ya kujiongezea kipato, Serikali inatakiwa iwawezeshe kiuchumi kwa kutoa mikopo mbalimbali na mikopo hiyo ifuate haki na usawa kwa makundi yote kama ilivyo hivi sasa mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Halmashauri kwa makundi ya Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu.
“Tushirikiane katika jamii kwa pamoja katika kuhakikisha tunajenga maadili bora kwa Vijana wetu wa sasa na siyo kuiachia Serikali peke yake katika kusimamia maadili ya Vijana wetu.” Alisema
Mada zingine zilizowasilishwa katika kongmano hilo ni pamoja na Rasilimali za Asili na Maendeleo endelevu, iliwasilishwa na Dkt. Grace Benedikito. Elimu na Teknolojia katika miaka63 ya Uhuru wa Tanzania Bara iliwasilishwa na Mwl.Deus Helman na Baraka Wambura.
Ndugu, Mtelela aliwapongeza na kuwashukuru watoa mada wote, pamoja, na washiriki walio changia mada mbalimbali zilizo wasilishwa katika kilele cha kongamano la maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
“Wazee wetu wametuanzishia Uhuru wa kiuchumi na sisi tunalo jukumu lakuhakikisha tunalinda amani na Uhuru tulio nao kwa kuhakikisha tunajipatia maendeleo yetu.”Alisema Ndugu, Mtelela
”Uongozi madhubutina Ushirikishwaji wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo Yetu”.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda