Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu. Oscar Jeremiah Nchemwa siku ya tarehe 10/1/2025 amefungua kikao cha kamati ya lishe cha kujadili mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Katika kikao, wajumbe kutoka idara mtambuka waliwasilisha bajeti zao na kuzijadili kuhusiana na masuala ya lishe, pamoja na kupanga mikakati ya namna gani wataboresha Afua za lishe kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, pamoja na wananchi wa halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Ndugu Nchemwa aliagiza idara mtambuka zinazosimamia masuala ya lishe shuleni na katika jamii kuhakikisha wanatenga bajeti ambayo itasaidia katika uboreshaji na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za lishe.
Naye, Afisa lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Bi.Saumu Abdallah aliomba bajeti ya lishe iliyokuwepo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kutokupunguzwa bali, ibaki kama ilivyo ama iongezeke kutokana na shughuli za lishe zitakavyotekelezwa.
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmahauri ya Wilaya ya Bunda, ambaye ni katibu wa kikao cha kamati ya Lishe alisema, lengo kuu la kuwa na mpango na bajeti ya lishe ni kwa ajili ya kuboresha Afya za watoto na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Kaimu Mkurugenzi alifunga kikao kwa kuwashukuru wajumbe wote waliohudhuria kikao na kusema, anaamini yale yote yaliyojadiliwa katika kikao yataenda kufanyiwa kazi na kutekelezwa katika kuhakikisha wanaboresha Afua za lishe.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda